Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 8, 2012

RAIS SHEIN AFUNGUA BARABARA YA AMANI HADI DUNGA


Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein amewataka wananchi kutomuonea haya mtu yeyote ambae anafanya kitendo kinachopelekea kuharibu barabara .
Amesema kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kwa ujenzi wa barabara ili kuwaondoshea wananchi kero za usafiri hivyo kufanya vyenginevyo sio jambo la busara na linarejesha nyuma maendeleo ya taifa .
Dk Shein ameyasema hayo leo huko Mwera wakati alipokuwa akifungua barabara mpya iliyotoka Amani Wilaya ya Mjini hadi Dunga Wilaya ya Kati iliyo na urefu wa kilomita 12.7 na upana mita 9 .
Amesema kuwa Barabara hiyo iliyojengwa na kampuni ya Mecco ya Dar-es –salam ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ( ADB) kwa kushirikiana na Serikali ya Mapiduzi ya Zanzibar, hivyo amewataka wananchi kuchukuwa jitihada ya kuitunza na kuwa ni walinzi kwa mtu yeyote ambae anaichafua barabara hiyo kwa namna yeyote ile ikiwamo upakizi mbaya wa nondo ambazo huninginia na kuharibu barabara ..
Aidha Dk Shein amelitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa uadilifu na kuepukana na tamaa za kupewa hongo na kuhatarisha maisha ya watu kwani kutokufanya hivyo ni kuweza kuwa jasiri katika kusimamia sheria za barabarani .
Pia Dk Shein amewataka Madereva wasiwe wanatumia barabara hiyo kwa kushindana jambo ambalo mara nyingi husababisha ajali zisizo na msingi wowote ule.
Mapema Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamadi Masuod ameeleza kuwa madhumuni makubwa ya ujenzi wa barabara hiyo ni kuwaondoshea kero wananchi na kusema kuwa daraja jipya lenye urefu wa mita 25 lililojengwa katika eneo la Mwera litaweza kutumika kwa muda usiopungua miaka mia moja iwapo litatunzwa vyema .
Amesema kuwa kwa ajili ya kuhifadhi historia ya Zanzibar Daraja la zamani litabakia na halitovunjwa na litaendelea kutunzwa na kutumika katika eneo hilo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...