Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 29, 2012

WEMA AMZODOA DIAMOND MCHANA KWEUPEE..!!
Hatimaye mrembo na msanii Wema Sepetu, ameweka wazi kuwa hataki tena kutembea na masharobaro kwani mapenzi yao yanakuwa hayana malengo zaidi ya kuchezeana.

Akizungumza hivi karibuni msanii huyu alisema kuwa msanii anayemfananisha na sharobaro ni aliyekuwa mpenzi wake
Nassib Abdul ‘Diamond’, kwani endapo angekuwa hayuko hivyo basi anaamini mapenzi yao yangedumu kwa muda mrefu.

Alisema kwa sasa anahitaji kutoka na mwanaume aliyemzidi umri kwani anaamini watu hao wanakuwa na mapenzi ya dhati tena hawana wivu kama watoto wadogo ambao muda wote hupenda kuwa karibu na wapenzi wao badala ya kufanya kazi.


“Kila kitu kina muelekeo wake, mapenzi yangu mimi na Diamond yangeweza kudumu lakini kutokana na usharobaro alionao ndiyo uliosababisha yote yaliyotokea, na ndiyo maana nasema kwamba ni bora kutembea na mwanaume aliyekuzidi umri mnaweza kufika mbali,”
alisema.

Msanii huyu alisema hata hivyo ni bora afunge ndoa na mwanaume atakayempata ambaye anajua maana ya mapenzi kuliko kutembea na vijana wadogo ambao hawajui nini maana ya mapenzi na hawana muelekeo wa maisha.

3 comments:

  1. WELL SAID WEMA,now you are talking.go mamy wangu,Mungu akusimamie upate Mume sasa.

    ReplyDelete
  2. smetime, beauty cheat...unajua wema, u are one of the pretty lady I ever see, how come u fell in luv with this tooons, jamani ulichemka sana, tena sana, kijamaa sijui kilitokea wapi, tandale kwa mtogole au mbagala, wewe dada yangu ukababaika na vijisenti vya bongo fleva while wewe ni international figure, hebu nyie wadada muwe na fikira mara mbili,how come ukampenda bongo fleva, sijui dada unapenda wanmuziki sana...acha hizi,umeharibu mbaaayaaa, acha hizo, nenda kanisani katubu zambi zako, acha kufunua nyeti zako, ujue thamani ya mwili wako, wewe ni sura na mfano wa mungu, tena mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu, jitunze utapata mume mzuri..mume bora hutoka kwa Mungu

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...