Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 12, 2012

MADA MAUGO KWENDA KUPAMBANA UJERUMANI BAADA YA KALAMA KUJIVUA UBINGWA WAKE


BAADA ya Shirikisho la ngumi za kulipwa Duniani (WBF) kumpokonya mkanda wake Karama Nyilawila sasa Shirikisho hilo linatazamia kumchukua bondia Mada Maugo ili kumuandalia pambano la ubingwa huo.

WBF jana ilimvua Nyilawila ubingwa huo baada ya kukacha kucheza pambano la kutetea mkanda huo alioupata tangu mwaka juzi, pambano lilopangwa kufanyika Februari 11 mwaka huu Ujerumani baada ya kuahirishwa kila mara.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Emmanuel Mlundwa alisema tayari ameishatuma picha za kwenye vitambulisho (Pasport size) za maugo WBF kwa ajili ya kutazamiwa kuandaliwa pambano hilo.

"Baada ya Nyilawila kuvuliwa ubingwa ni kawomba waandae pambano kwa ajili ya bondia mwingine wa Tanzania wakakataa lakini nilivyowaomba wakaniambia nitume paspoti size za bondia ninaemuona anauwezo nikawatumia za Maugo hivyo mchakato unaendelea kuhusu kumuandalia pambano hilo," alisema Mlundwa.

Alizungumzia kuvuliwa ubingwa kwa Nyilawila alisema, tatizo sio kwa Nyilawila kwani hata yeye anatafuta riziki lakini lawama anawatupia TPBC kwa kukubali kumpa kibali cha kuandaa pambano hilo, promota Philemon Kyando kitu ambacho PST na TPBO waliamua kumnyima kwa manufaa ya mchezaji.

"Kyando alikuja kuomba kibali cha kuandaa pambano la Nyilawila na Cheka tukamnyima kutokana na kumlinda Nyilawila asinyang'anywe ubingwa kwa kucheza pambano hapa nchini la TPBC hawakutambua uthamani huo na kuamua kumpa sasa baada ya kuona kavuliwa ubingwa ndio wakanipiga wakidai kushtushwa na taarifa hizo kitu ambacho kinakuja wakati usio rasmi," alisema Mlundwa.

Aliongeza kuwa, Nyilawila alimtumia ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake (SMS) kuwa ameamua kuachia mkanda huo ambapo yeye alimtumia muwakilishi wa WBF na kushirikiana na Shirikisho hilo wakatangaza kumnyang'anya mkanda huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...