Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 5, 2012

HAMAD RASHID NA WENZAKE WATATU WATIMULIWA CUF WAVULIWA UANACHAMA


BARAZA Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) limemvua uanachama Mbunge wa Wawi na Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, Hamad Rashid Mohamed, kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama na hivyo kupoteza sifa za uanachama. Akitangaza uamuzi huo katika Hoteli ya Manson Mji Mkongwe jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro alisema mbali na Hamad Rashid, pia baraza hilo limewavua uanachama wajumbe wengine watatu wa Baraza Kuu. Wajumbe hao ni Doyo Hassan Doyo kutoka katika Mkoa wa Tanga, Juma Sanani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na Shoka Khamis Juma, aliyewahi kuwa Mbunge wa Micheweni kwa tiketi ya CUF. “Baraza Kuu la CUF limewafukuza viongozi hao baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili kutoka wajumbe wa Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka wajumbe Zanzibar,” alisema Mtatiro. Mjumbe mwingine: Yasin Mrotwa amepewa onyo kali na karipio na kwa mujibu wa Mtatiro, anaendelea kuchunguzwa na Baraza Kuu. Seif dikteta! Baada ya kuvuliwa uanachama, Hamad Rashid alizungumza na waandishi wa habari na kumuita Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, dikteta na kiongozi asiyeheshimu uamuzi wa Mahakama. “Sisi tumeweka pingamizi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa mkutano wa Baraza Kuu na hati ya Mahakama ipo wanayo...sasa nawashangaa wanakiuka sijui kwa nini?” Alihoji Hamad Rashid. Alisema watakwenda tena mahakamani Februari 14 kusikiliza shauri lao la pingamizi la kikao hicho. Wengine boya fuata upepo Alipoulizwa kama anakubaliana na uamuzi wa kikao hicho, alisema anapinga kwa sababu CUF kwa muda wote imekuwa ikiongozwa na Maalim Seif tu; ndiyo mwenye uamuzi na waliobakia wanafuata upepo. “CUF ni Maalim Seif tu...waliobakia wote ni boya hawana uamuzi wa aina yoyote ndio maana chama chetu kinaitwa CCM B kwa sababu kinakwenda kinyume na mwelekeo uliokuwepo awali. UCCM B na Umakamu wa Rais! “Chama kinafuata sera za CCM si unaona hata Maalim Seif sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais yumo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Hamad. Mtatiro alipoulizwa kuhusu kupokea hati ya mahakama alisema hawaitambui kwani inaweza kuandikwa na mtu yeyote yule. Maalim ni Bwana Mkubwa Naye Shoka alisema CUF sasa inaelekea kubaya kwa sababu imekuwa na uamuzi ya upande mmoja tu kutoka kwa Bwana Mkubwa Maalim Seif. 'Chama sasa kinaelekea kubaya...maamuzi yote ya chama yanatoka kwa Maalim Seif tu....mimi nimemwambia kwamba amezoea kuwafukuza wanachama wenzake na iko siku atafukuzwa yeye,” alisema Shoka. Alipoulizwa kama atahama CUF au atabaki kuwa muumini wake, alijibu kwamba ataangalia mustakabali wa baadaye. Yalipoanzia Mtafaruku ndani ya chama hicho ulianza pale Hamad Rashid, alipoulaumu uongozi na mwenendo wa chama hicho, akisema kuwa Maalim Seif inafaa aache dhamana ya ukatibu mkuu wa chama. Kwa habari zaidi bofya hapa:http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/hamad-rashid-atimuliwa-cuf

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...