Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 9, 2016

MABONDIA FRANSIC MIYEYUSHO NA NASSIBU RAMADHANI KUZIPIGA SIKU YA PASAKA UWANJA WA TAIFA

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kiongozi wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu kuwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Cristopher Mzazi wakati wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS 

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano utakaokuwa kama ndio mkali wa kufungua mwaka 2016

aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga siku ya pasaka

Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba

Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kwa wingi kushudia mpambano uho ambao utakuwa na msisimko wa aina yake vilevile wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wawai kurudi majumbani kwa na kujumuika na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema ili ngumi nazo zianze kwa wakati na kumalizika kwa wakati


siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali







Thursday, February 4, 2016

MABONDIA MADA MAUGO NA ABDALLAH PAZI KUONESHANA UBABE UWANJA WA NDANI WA TAIFA SIKU YA PASAKA




Mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa Dar es salaam katikati ni mratibu wa mpambano uko kochwa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mratibu wa mpambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka utakaofanyika  uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Mada Maugo akikabiziwa mkataba wake na mratibu wa mapambano wa masumbwi  Rajabu Mhamila 'Super D' kati yake na Abdallah Pazi mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka  katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Abdallah Pazi kushoto akipokea sehemu ya fedha yake kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika uwanja wa ndani wa taifa anaetoa fedha hizo ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS




Bondia Abdallah Pazi kushoto akipokea mkataba wake kutoka kwa mratibu wa mpambano uho  Rajabu Mhamila 'Super D'  baada ya kusaini kwa ajili ya kupigana na Mada Maugo siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Mada Maugo kushoto akipokea sehemu ya malipo ya awali kutoka kwa mratibu  Rajabu Mhamila 'Super D' wa mpambano wake na Abdallaha Pazi. utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

Mabondia Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa   taifa mpambano wa raundi nane KG 76.

akizungumza wakati wa kutiliana saini mikataba hiyo kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ni mratibu wa mpambano uho

amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo ambao wanatamba katika tasnia ya masumbwi nchini

ili wapenzi wa mchezo wa masubwi waburudike siku hiyo ya sikukuu ya pasaka

mbali na mpambano uho siku hiyo bondia chipkizi anaekuja kwa kasi zaidi katika mchezo wa masumbwi Vicent Mbilinyi anaetokea katika Super D  Boxing Promotion atakae pambana na Mwinyi Mzengela mpambano wa KG 63 raundi nane mpambano mwingine utawakutanisha bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba
 

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali


TIGO YAWAPA WATEJA WAKE HUDUMA YA WHATSAPP BURE

????????????????????????????????????Uzinduzi rasmi
New Picture
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam .
New Picture (1)
Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
New Picture (2)
Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
New Picture (3)
Ni kama wanasema ‘tumependeza sana ngoja tujipige picha’ wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
New Picture (4)
Wageni waaalikwa wakiwa katika maski za ” Emojis ” wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
New Picture (5)
Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
New Picture (6)
Washereheshaji katika uzinduzi huo,Mc Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure.
New Picture (7)
Burudani ikiendelea kutoka kwa wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
New Picture (8)
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za “Emojis ” wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
New Picture (9)
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
New Picture (10)
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) Meneja wa gharama wa Tigo Jakhangic Tulaganov na Meneja masoko Olivier prentout wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency
New Picture (11)
Bloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile ‘Joti’ wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency.
………………………………………………………………….
Dar es Salaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.
Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.
Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na duniani inatumiwa na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.
“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE. Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.
Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho anaweza kukipata kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.
WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.

KASI YA RAIS MAGUFULI YAGONGA MWAMBA POLISI MLANDIZI


Kituo cha Polisi cha Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani.
…………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
ASKARI wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani, Kituo cha Polisi Mlandizi
wamewasotesha kwa takribani masaa mawili  na nusu wanahabari kupata risiti
ya malipo ya faini aliyotozwa dereva wao baada ya kudaiwa kufanya kosa la
kutaka kulipita gari lingine sehemu isiyoruhusiwa.
Sakata hilo lilianza wakati polisi alipolisimamisha gari hilo katika Kituo cha
Visiga, Mlandizi, wilayani Kibaha, Pwani ambapo alimuomba dereva leseni yake
na kumuamuru ateremke ili ajieleze akiwa nje ya gari na hatimaye kumlipisha
faini ya sh. 30,000 kwa kosa hilo.
Baada ya wanahabari waliokuwa kwenye gari hilo kumsubiri dereva kwa
takribani nusu saa, waliamua kuteremka kumfuata kujua kinachoendelea, kwani
walikuwa wana haraka ya kufika Dodoma muda waliopangiwa  ili waungane na
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda Singida kwenye
maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM.
Lakini baada ya mmoja wao kuwauliza Trafiki sababu zinazosababisha
kutomwachia dereva, walijibu kwa kashfa na kejeli, wakihoji kwani nyie ni akina
nani? na dereva wenu asipolipa faini basi watakaa hapo kituoni hadi jioni.
Mmoja wa wanahabari hao alilipa faini ya sh. 30,000 na kuomba risiti.
Hapo ndo songombingo ilianza ambapo Trafiki wa kike alijibu kuwa  hawana
risti bali kinachofanyika pale ni kuandikiwa tu taarifa ya kosa lao na kwenda
Kituo cha Polisi cha Mlandizi kilichopo takribani umbali wa Km 5, na wengine
waliokamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani waliamuliwa
kwenda kupata risiti katika kituo hicho.
Mabishano makubwa yalitokea hapo baina ya Trafiki na wanahabari waliokuwa
wanahoji ni kwa nini kitabu cha risiti wala mashine za kielekroniki havipo hapo
ili kurahisisha kazi. Askari wa kike na mmoja wa kiume walijibu kuwa
wasifundishwe kazi.
“Msitupotezee muda hapa, nendeni Mlandizi, mkapate hiyo risiti,”alisema trafiki
wa kike. Wakati anasema hivyo kumbe mhasibu wao alikuwepo palepale Visiga,
lakini bila kuwaambia ondokeni naye ili akawahudumie.”
Pia, mmoja wa Trafiki aliuponda sana utaratibu wa wakosaji kulipia faini kwa
kutumia mashine za elekroniki akidai kwamba ni hasara kwa trafiki na madereva
ni bora mashine hizo ziishie Dar es Salaam zisipelekwe Mkoa wa Pwani.Trafiki
wengine walisikika wakisema kuwa hivi hawa jamaa wanaolazimisha kupewa
risiti ni akina nani, waache waende zao, wakafie mbali.
Maneno hayo yalionekana kuwaudhi wanahabari na kuamua kuondoka kwenda
Kituo cha Polisi Mlandizi, kufuatilia risiti, lakini walichokikuta huko ni maajabu,
hasa ya kuambiwa kuwa Mhasibu hayupo ofisini kwake amekwenda kununua
peni.
Baada ya wanahabari hao kusubiri kwa takribani saa moja, waliamua kwenda
kaunta kuulizia na kuomba kuzungumza na Mkuu wa Kituo ili awasaidie kupata
risiti wawahi kwenda Dodoma, lakini mmoja wa askari aliyekuwa zamu aliwajibu
kuwa Mkuu wa Kituo hajafika ofisini amepitia Kibaha Mjini kwenye mkutano.
Alipoombwa awasaidie kumpata mhasibu, askari huyo alitoka nje hadi ofisi ya
Mhasibu alipomkosa akaamua kumpigia simu na kuwajibu kuwa ametoka mara
moja kwenda kununua peni. Jambo hilo liliwashangaza sana wanahabari na
kuanza kuhoji kwamba iweje kitendo cha kununua peni  kitumie muda wote huo
na kusababisha watu wakiwemo wao kukosa huduma tena asubuhi majira ya
saa 3?
Mmoja wa wananchi aliyekwenda kituoni kupata huduma ya risiti, alisikika
akilalamika kuwa tabia hiyo ya kuchelewesha kutoa huduma ipo sana kituoni
hapo na kwamba wanaoonekana kabisa hawaendani na kasi ya kufanya kazi
anayoitaka Rais Dk  John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.
Mle ndani ya Kituo cha Polisi walisikika wakiulizana kwamba hivi haw watu
wanaowasumbua na kutaka kuzungumza na mkuu wa kituo ni akina nani hawa,
eti wanataka risiti, ebu tumpigie simu mhasibu aje atuondolee balaa hapa.
Baada ya muda askari mwenye E 3275 alitoka nje na kuwaambia wanahabari
kuwa mhasibu amepigiwa simu atakuja muda si mrefu mhudumiwe muondoke,
lakini mmoja wa wanahabari hao anayemiliki blogu ya Full Shangwe, John
Bukuku,  alihoji kuwa hivi ni kwanini polisi wa kituo hicho hawaendani na kasi
ya Rais Dk. Magufuli? alijibu kuwa kwani kuna nini?
Baada ya muda Mhasibu aliwasili kwa Bodaboda, na alipofika aliwakebehi
wanahabari kwamba anawashangaa kwa yeye kumuacha kule Visiga
alikokuwa nao na kuwahi kituoni, ndipo wanahabari nao wakashangaa kumuona
tena kituoni hapo wakati wlipofika kituoni waliambiwa ameenda kununua peni.
Dereva alimwambia haya twende ukachukue risiti yako muondoke na
watu wako. Dereva aliingia na kupatiwa risiti kutoka kwenye kitabu kipya
ambacho kwa mujibu wa dereva kilionekana dhahiri kuwa ni kipya.
Lakini kwa masaa yote waliyokaa wanahabari kituoni hapo (takribani masaa
mawili), hawakuwaona madereva wa magari waliokamatwa pamoja na gari lao
na kuandikiwa makosa na faini pale Visiga, hawakufika Kituo cha Polisi
kupatiwa risiti, kitendo ambacho kinaashiria fedha wanazolipishwa madereva
kwa kutenda makosa hazitolewi risiti, hivyo mapato ya serikali kupotelea
mifukoni mwa baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani.
Baada ya wanahabari hao kupata risiti majira ya saa 4:15 waliamua kuondoka
kituoni hapo kuanza safari ya kwenda Dodoma kuwahi msafara wa Katibu Mkuu
wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana uliokuwa unawasubiri kwenda Singida.

Tuesday, February 2, 2016

BONDIA YUSUPH MWEGELO HAPANIA KUMCHAKAZA DEI MBAISO FEB 14



Bondia Yusuph Mwegelo katikati akimtupiana makonde na Mohamed Muhunzi wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupigana na Dei Mbaiso feb 14 katika ukumbi wa musoma bar Tandika  kulia ni kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Yusuph Mwegelo katikati akimtupiana makonde na Mohamed Muhunzi wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupigana na Dei Mbaiso feb 14 katika ukumbi wa musoma bar Tandika  kulia ni kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Yusuph Mwegelo kulia akimtupiana makonde na Mohamed Muhunzi wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupigana na Dei Mbaiso feb 14 katika ukumbi wa musoma bar Tandika  kulia ni kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimnowa bondia Yusuph Mwegelo anaejiandaa na mpambano wake wa Feb 14 katika ukumbi wa musoma bar ambapo atakumbana na Dei Mbaiso Picha na SUPER D BOXING NEWS

Monday, February 1, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI APIGIA MKWALA MZITO MWINYI MZENGELA KUPIGANA PASAKA

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amemchimbia mkwala mkali bondia Mwinyi Mzengela watakapokutana siku ya April 26 katika sikukuu ya Pasaka 

Mbilinyi amemtangazia kiama Mzengela baada ya kukubali kupambana nae katika uzito wa KG 63 amesema nitamsambalatisha mapema mno bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa KG 63 kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC)

Mbilinyi aliongeza kwa kusema namuheshimu Mzengela kwa kuwa ni bingwa wa Taifa ata hivyo nita akikisha nausambalatisha utawala wake na mimi nakuwa juu yake kwa kuwa nia ninayo uwezo ninao na nitaonesha jinsi ngumi zinavyochezwa  

najuwa katika ngumi za kulipwa sina mda mrefu sana na nimeshatambulika kwa kuwa najua nini nakifanya katika mchezo uhu wa masumbwi nchini

nimeingia katika ngumi za kulipwa sio kupoteza mda kwa kuwa najua mchezo wa ngumi ila kwangu mimi ni ajira na ndio ninayo itegemea

Airtel Fursa yachanja mbuga


Mkurugenzi  wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu  muendelezo na msimamo wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 katika ofisi za Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam ili kuendelea kuwezesha  vijana wengi nchini.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Airtel FURSA kutumia Simu kuwafikia vijana nchi nzima

AWAMU ya pili ya mpango wa Airtel FURSA imezidi kujimarisha nchini baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kujipanga kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kutumia mtandao wa Airtel kuwafikia vijana nchi nzima kwa njia ya simu.

Akizungumza jijini hapa mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano, alisema mafunzo yajayo ya semina zinazoendelea kwa vijana wajasiriamali yatafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Lindi.

“Pia wakati wowote kuanzia sasa Airtel FURSA tutaweka wazi mfumo wa mafunzo kwa njia mpya ya kiubunifu zaidi  kwa njia ya simu za mkononi ili kuwafikia vijana wengi zaidi wanaokabiliwa na changamoto za ajira,” alisema Bi, Singano.

Alisema walengwa wa mpango huo ni vijana wenye kati ya umri wa miaka 18 na 24 na kwamba tangu mradi huo uanze mwaka jana na kudumu kwa miezi sita, takribani vijana 2,500 nchini wamekwishafaidika na sasa wanamiliki biashara na miradi mbalimbali.

Mkurugenzi huyo wa Airte Bi, Beatrice Singano  aliwaomba wadau na serikali kujitokeza na kushirikiana na Airtel kuwawezesha vijana ili nao waweze kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.

“Katika msimu huu wa pili wa Airtel FURSA, tutawafikia vijana wengi zaidi na kuwapa mafunzo na semina, ushawishi na kuwainua kwa misaada ya vitendea kazi.

“Tayari tumefika na kutoa mafunzo katika mikoa ya Manyara na Morogoro, sasa  tunaingia Dodoma, kisha vijana wa Lindi na Dar es Saalam wajiandae,” alisema.

Alisema uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa njia ya simu utawezesha hata wale wasio na nafasi ya kuhudhuria mafunzo na semina, wataweza kufanya hivyo popote walipo.

“Tunaamini kuwa msimu huu utakuwa na mafanikio zaidi kwani wengi watawezeshwa kupitia programu hii,” alisema

Mpango wa Airtel FURSA ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa, mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kwa njia tofauti waweze kufikia malengo yao.

Pia mpango huu unawawezesha vijana kuongeza mitaji au kupanua biashara zao za ujasiriamali kwa kuwapa msaada wenye thamani ya hadi Sh. milioni 10 kwa kila mmoja.


Ili kijana kufaidika na msaada huo, anatakiwa kutuma maombi kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 15626 akiwa jina kamili, umri wake, aina ya biashara anayoifanya, mahali alipo na namba za simu, au kupitia airtelfursa@tz.airtel.com au kujaza fomukutoka kwenye tovuti www.airtel.com.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA AISHUKURU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, WANANCHI WA KINONDONI JIJINI DAR


DC. Paul Makonda
Mnamo tarehe 23 wilaya yangu iliamua kufanya upimaji wa bure wa magonjwa ya moyo, upimaji ambao niliamini ungebeba faida kubwa nne: moja, kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara miongoni mwa wananchi, pili kubaini watu ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, tatu kuchukua hatua za awali za kuwasaidia wale ambao tayari wameshashambuliwa na magonjwa hayo na mwisho kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yote ya moyo. 


Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa unaoweza kuzalisha magonjwa mengi sana na kama hujafanya vipimo sahihi ni rahisi kushughulika na matokeo ya ugonjwa huku ukiacha chanzo kikizaa magonjwa mengine. Mathalani, unaweza kujikuta unahangaika na kuvimba kwa miguu au kuhangaika na macho ama figo aukisukari na hata kupoteza nguvu za kiume ukifikiri ndio tatizo kumbe tatizo la msingi ni moyo. 



Kimsingi ni kwasababu hizo nilizozianisha nilichukua hatua ya kukiomba taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kinachosimamiwa na Profesa Janabikinisaidie kutoa huduma hiyo bure ndani ya wilaya yangu.



Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza sana madaktari kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na mwananyamala kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu kulifanya zoezi hilo. zoezi ambalo lilikuwa kubwa na zito kwani kwa makadirio ya awali tulitegemea kupata watu wasiozidi 2000 ila badala yake walijitokeza wananchi zaidi ya 7000 ila kutokana na umahiri wa madaktari hao tuliweza kuhudumia zaidi ya wananchi 5900 ingawa tulilazimika kulifanya zoezi hilo kwa siku ya pili yake ambayo ilikuwa ni tarehe 24. 



Na kwa watu wengine zaidi ya 1200 waliokuwa wamebaki, zoezi lao tulilipanga na kulifanya tarehe 30 ya mwezi huu huu wa kwanza. Ukweli ni kwamba, mambo mengi yalijitokeza kwa siku hizi tatu za upimaji; wapo waliolazimika kukimbizwa kwa ambulance kuelekea hospitali za mwananyamala na muhimbili, wapo waliolazimika kupewa appointments za kuwaona madaktari, wapo waliopewa ushauri wa matumizi ya dawa na wengine kubadilishiwa dawa sambamba na maelekezo ya utumiaji wa chakula na ufanyaji wa mazoeziili kupunguza uzito. 



Nichukue tu fursa hii kuwapongeza wanakinondoni kwa kuitikia wito na kuniamini mkuu wao wa wilaya na serikali yangu kwa ujumla kwamba tuna nia njema na tunawapenda wananchi wetu kwa kuwahakikishia afya zao zinastawi na kuendelea kuwa bora siku zote. 



Kutokama na maelezo niliyoyatoa hapo juu sambamba na sababu zilizonisukuma kufanya zoezi hilo na kutokana na muitikio mkubwa wa wananchi bila kusahau matokeo ya vipimo vilivyofanyika na kupata majibu ya kwamba watu wengi wanahitaji matibabu, kubadilishiwa dawa, maelekezo ya matumizi sahihi ya vyakula pamoja na mazoezi nimefanya uamuzi wa kulifanya zoezi hili la kudumu na tayari nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na nimetafuta njia na utaratibu bora zaidi wa kulifanya zoezi hili kuwa ni zoezi la kudumu.



Sasa basi, natamka rasmi kuwa serikali ya wilaya ya kinondoni inaanza utaratibu wa kupima bure mara tatu kwa mwaka, utaratibu ambao utaanza katikati ya mwezi wa nne. Zoezi hili litafanyika kwa kupima zaidi ya magonjwa kumi ikiwemo yafuatayo: moyo, kisukari, kansa, macho, figo, meno, kifua kikuu (TB), typhoid, magonjwa ya ngozi, presha, animonia, kansa ya kizazi, kansa ya matiti, mabusha na matende. 



Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, nimeshafanya mazungumzo na hospitali kubwa na kila hospitali itatoa vitengo viwili au vitatu na utaratibu utakuwa hivi. Kwa mfano, utakuta banda limeandikwa Jakaya Kikwete Cardiac Institute ndani ya banda hilo utakuta madaktari waliobobea kwenye upande wa moyo na upimaji wa presha kwahiyo mtu anayetaka kupima moyo ama presha atakwenda moja kwa moja kwenye banda husika. 



Ama unaingia kwenye banda limeandikwa Ocean Road hospital kwahiyo yeyote anayetaka kupima kansa ataingia humo…hivyo hivyo kwa magonjwa mengine yote: kutakuwa na mabanda tofauti yaliyoandikwa ni hospitali gani na wanapima magonjwa gani, lengo ikiwa ni kumpa urahisi mpimaji atakayejitokeza. 



Mwisho ila si kwa umuhimu niwashukuru sana wananchi wote wa wilaya nyingine na wale waliotoka mikoa mbalimbali ikiwemo Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi na Dodomakwa imani yao kubwa juu ya tukio hili iliyowafanya kutoka mbali na kujisogeza mpaka viwanja vya leaders wakiwa na imani ya kupatiwa huduma hata kama zoezi hili lilikuwa limewalenga wakazi wa wilaya ya Kinondoni. 



Sambamba na kuwashukuru wananchi niwashukuru pia waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari mbele kulitangaza tukio na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kwa wakati. 

Imetolewa na:- Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda

TANROAD YA BOMOA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKA HIFADHI YA BARABARA MAENEO YA BUZA, LUMO TEMEKE JIJINI DAR


 Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana. Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.
 Wakazi wa Buza Sigara wakiondoa mabaki ya mbao baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), kubomoa nyumba hizo.
 Kijana akipita jirani na nyumba iliyobomolewa.
 Mkazi wa Buza akiondoa mabaki ya mbao baada ya nyumba yake kubomolewa.
 Moja ya nyumba iliyobomolewa.
 Wananchi wakiangalia moja ya Baa iliyobomolewa.
 Tingatinga likiwa kazini.
 Watoto wakiangalia zoezi la ubomoaji lilivyokuwa likiendelea.
 Ofisa wa Tanroad akisimamia ubomoaji huo.
 Wananchi wakiangalia zoezi la ubomoaji.
 Tingatinga likiisambaratisha moja ya nyumba iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara eneo la Buza kwa Lulenge.
 Wananchi wakiangalia  ubomoaji huo.

MABONDIA MOHAMEDI MATUMLA NA COSMAS CHEKA WASAINI KUZITWANGA SIKUKUU YA PASAKA


Bondia Cosmas Cheka akipokea mkataba wake wa kuzipiga na Mohamed Matumla siku ya sikukuu ya Pasaka kutoka kwa mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kutiliana saini ya kuzipiga siku ya sukukuu ya Pasaka katikati ni mdau wa masumbwi nchini Abdallah Mwasora Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto ambaye ni mklatibu wa  mpambano wa bondia Mohamed Matumla kulia atakaepambana na Cosmas Cheka akikabidhiwa mkataba wake pamoja na sehemu ya malipo ya mchezo wake utakaochezwa siku ya  sikukuu ya Pasaka jijini Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Mohamed Matumla  akisaini mkataba wake wa kuzipiga na Cosmas Cheka siku ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akimwesabia kiasi cha fedha ambacho alikabidhiwa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake



Bondia Cosmas Cheka kushoto akitia saini mkataba wa kuzipiga na Mohamed Matumla mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka kulia ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Cosmas Cheka kushoto akihesabu sehemu ya fedha zake kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Mohamed Matumla utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka  kutoka kwa mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D'  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Cosmas Cheka na Mohamed Matumla wamesaini kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka uzito wa kg 61 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa

akizungumza baada ya kutiliana saini ya mikataba kwa mabondia hawo

Mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema nimewasainisha mabondia Mohamed Matumla atakaezipiga na Cosmas Cheka ata hivyo nipo kwenye mazungumzo na mabondia Fadhili Majia na Nassibu Ramadhani ambao nilikuwa ningie nao mikataba ata hivyo kambi hizo mbili wametofautiana kiswahili kuusiana na mikataba hiyo ata hivyo naendelea kushawishi kambi zote mbili ziwe katika msimamo ambano tumekubaliana ili tufanye kazi

mana tulikuwa tusaini mpambano uho leo rakini mezani nilikuwa na kambi moja tu ya Ramadhani hivyo atukuweza kuelewana na kambi ya Majia

wakati uho uho bondia Vicent Mbilinyi atatwangana na Mwinyi Mzengela katika mpambano wa raundi nane uzito wa kg 63 

na bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atakumbana na Twaha Kiduku mpambano wa raundi nane uzito wa kg 63


siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...