Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 9, 2016

MABONDIA FRANSIC MIYEYUSHO NA NASSIBU RAMADHANI KUZIPIGA SIKU YA PASAKA UWANJA WA TAIFA

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kiongozi wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu kuwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Cristopher Mzazi wakati wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS 

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam

akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano utakaokuwa kama ndio mkali wa kufungua mwaka 2016

aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga siku ya pasaka

Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba

Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kwa wingi kushudia mpambano uho ambao utakuwa na msisimko wa aina yake vilevile wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wawai kurudi majumbani kwa na kujumuika na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema ili ngumi nazo zianze kwa wakati na kumalizika kwa wakati


siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed AliNo comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...