Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 1, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI APIGIA MKWALA MZITO MWINYI MZENGELA KUPIGANA PASAKA

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amemchimbia mkwala mkali bondia Mwinyi Mzengela watakapokutana siku ya April 26 katika sikukuu ya Pasaka 

Mbilinyi amemtangazia kiama Mzengela baada ya kukubali kupambana nae katika uzito wa KG 63 amesema nitamsambalatisha mapema mno bondia huyo ambaye ni bingwa wa uzito wa KG 63 kupitia Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC)

Mbilinyi aliongeza kwa kusema namuheshimu Mzengela kwa kuwa ni bingwa wa Taifa ata hivyo nita akikisha nausambalatisha utawala wake na mimi nakuwa juu yake kwa kuwa nia ninayo uwezo ninao na nitaonesha jinsi ngumi zinavyochezwa  

najuwa katika ngumi za kulipwa sina mda mrefu sana na nimeshatambulika kwa kuwa najua nini nakifanya katika mchezo uhu wa masumbwi nchini

nimeingia katika ngumi za kulipwa sio kupoteza mda kwa kuwa najua mchezo wa ngumi ila kwangu mimi ni ajira na ndio ninayo itegemea

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...