Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 19, 2016

BONDIA FRANSIC CHEKA ATAMBA KUMDUNDA MSERBIA GEARD AJETOVIC

Bondia Fransic Cheka 'katikati' akiwa katika picha ya pozi na meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited baada ya kuzunumzia mpambano wake na Mserbia Geard Ajetovic utakaofanyika 
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni meneja msaidizi Nassoro Said 'mzee wa mbele
 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Msanii wa bendi ya muziki wa dansi African Stars 'twanga pepeta' Luiza Mbutu kulia akizungumza na waandisho wa habari awapo pichani wakati wakitangaza mpambano wa bondia Fransic Cheka na Mserbia Geard Ajetovic utakaofanyika 
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katikati ni msanii Ally Choki na kushoto ni promta Jay Msangi
Picha na SUPER D BOXING NEWS


Meneja wa Cheka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile kushoto akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya mpambano wa bondia Fransic Cheka katikati kulia ni promota Jay Msangi
mpambano wa Cheka na Mserbia Geard Ajetovic utakaofanyika 
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27
Bondia Fransic Cheka  kushoto akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpambano wake na  Mserbia Geard Ajetovic utakaofanyika 
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katikati ni meneja wake
Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile  na promota Jay Msangi
Picha na SUPER D BOXING NEWSSUPER D KUSHOTO NA FRANSIC CHEKA

Na Mwandishi Wetu

BONDIA maarufu nchini  Francis Cheka na Mserbia, Geard Ajetovic.watazipiga katika
Pambano  la raundi 12 la kuwania ubingwa wa mabara wa WBF la uzani wa super middle limepangwa kufanyika kwenye viwanja vya Leaders Dar es Salaam ambapo bendi ya Twanga Pepeta itatoa burudani.
Meneja wa Cheka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile alisema Jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na Waziri Nape ameridhia kuwa mgeni rasmi siku hiyo.
Kwa mujibu wa Ndambile, mpinzani wa Cheka atawasili Jumatano hii sanjari na wawakilishi kutoka Shirikisho la ngumi la dunia (WBF) wakiongozwa na Rais wake, Goldberg Haward ambao watawasili Alhamisi hii.
"Maandalizi yote yamekamilika, Serikali Yetu imetusapoti kwa namna ya pekee na Waziri wa Michezo ameridhia kuwa mgeni rasmi siku hiyo.
"Kabla ya Cheka kupanda ulingoni, kutakuwa na burudani ya bendi ya Twanga Pepeta na pambano rasmi litaanza saa moja Jioni ," alisema.
Akizungumzia pambano hilo, Cheka alisema yuko fiti na kusisitiza  hajawahi kuwaangusha Watanzani hivyo wajitokeze kumpa sapoti.
"Nimefarijika kuona Waziri wa Michezo anakuja kunisapoti, nimuombe pia hata Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) aje alishuhudie na waahidi Watanzania sitawaangusha," alisema Cheka.
Cheka na Ajetovic watazichapa kwa Mara ya pili jijini Dar es Salaam baada ya Mara ya kwanza nchini England mwaka 2008 na Cheka kupigwa kwa pointi.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile


Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...