Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 19, 2016

Airtel yachezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akiongea na wateja wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika  ambapo wateja 40 walichaguliwa kuwa washindi wa promosheni hiyo. Pichani ni Mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha, Bakari Majid na Afisa masoko wa Airtel Nasoro Abdulbakari (kulia).
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akimkabithi mshindi wa  Airtel Mkwanjika Diana Samwel na mkazi wa Dar es Saalam pesa taslimu mara baada ya kujinyakulia shilingi 480,000 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika. 
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

·  Zaidi ya wateja 212 wajishindia pesa taslimi

Dar es Salaam  

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika nakupata washindi 40 ambapo kila mmoja atajishindia pesa taslimu hadi shilingi milioni 1 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika

Promosheni ya Airtel Mkwanjika ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Disemba na kuwazawadia wateja wanne watakaojiunga na vifurushi vya yatosha au kuongeza  muda wa maongezi kupitia vocha au Airtel Money kila siku. Jumla ya washindi 28 walipatikana kupitia droo kila wiki na kuzawadiwa pesa taslimu.

Akiongea wakati wa kuchezesha droo ya mwisho, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema”  Leo tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya Airtel Mkwanjika , promosheni ambayo imeweza kuwazawadia wateja zaidi ya 212.

nchi nzima.  Tunajisikia furaha kuona mwitikio mkubwa  kutoka kwa wateja wetu na tunapenda kuwahakikishia kuwa Airtel itaendelea kutoa huduma bora za kibunifu  zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu yanayoendelea kubadilika na kukua kila siku na  huku tukiendelea kuwazawadia kupitia promosheni kama hii ya Airtel Mkwanjika”

“Tunaamini kupitia Airtel Mkwanjika tumetoa zawadi ambazo zimewawezesha wateja wetu kukabiliana na changamoto walizonazo na kuwasaidia  kuongeza mitaji ya biashara zao na  kuongeza ufanisi katika  shughuli zao mbalimbali za kiuchumi na za kijamii. Tunaamini washindi wetu watakuwa ni ushuhuda tosha wa namna gani Airtel kupitia promosheni hii imeweza kubadili maisha yao na ya jamii zao kwa ujumla. Aliongeza Matinde

Promosheni ya Airtel Mkwanjika imefikia mwisho, Airtel bado itaendelea kuwawezesha washindi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini  ambao bado hawajaingia kwenye  boksi la Airtel Mkwanjika kupata nafasi ya kufanya hivyo ili kuweza kujiokotea pesa na kukabithiwa zawadi zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...