Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 26, 2016

MABONDIA KUTWANGANA KESHO LEADERS CLUB KESHO NI CHEKA NA AJETOVIC


Bondia Lulu Kayage kushoto akinuliwa juu mkono na Promota Jay Msangi baada ya kupima uzito wakati mpinzani wake Mwanne Haji akiinuliwa mkono na Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited ambaye ni mlatibu wa mpambano uho kulia kabisa ni Rashid Nassoro 'Mzee wa Mbele' mdau wa mchezo wa ngumi picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Lulu Kayage akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na mwanne Haji kesho jumamosi ya feb 27 kulia ni Emanuel Mlundwa picha na SUPER D BOXING NEWS

Luilu Kayage

Bondia Mwanne Haji akipima uzito kwa ajili ya mpambano weake na Lulu Kayage kulia picha na SUPER D BOXING NEWS

  • Mabondia Lulu Kayage kushoto akitunishiana misuli na Mwanne Haji baada ya kupima uzito kwa ajili a mpambano wao kesho katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni picha na SUPER D BOXING NEWSMabondia Fransic Cheka kulia akitunishiana misuli na Mserbia Geard Ajetov baada ya kumia uzito kwa ajili ya mpambano wao kulia ni mdau wa mchezo wa ngumi Nassoro Rashidi na
meneja wake cheka, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Securit
picha na SUPER D BOXING NEWS


Mabondia Fransic Cheka kulia akitunishiana misuli na Mserbia Geard Ajetov baada ya kumia uzito kwa ajili ya mpambano wao kulia ni mdau wa mchezo wa ngumi Nassoro Rashidi na
meneja wake cheka, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Securit
picha na SUPER D BOXING NEWS

CHEKA AKIPIMA UZITO
Bondia Shabani Kaoneka akipima uzito kwa ajili ya mp[ambano wake kesho

 NA MWANDISHI wetu
 MABONDI fransic Cheka na Geard Ajetovic  wamepima uzito kwa ajili ya pambano lao la mabara la uzito wa super middle la Shirikisho la Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF)   ambapo  waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,  atawaongoza Watanzania kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, kushuhudia pambano la ubingwa wa Mabara wa WBF Intercontinental kati ya Francis Cheka na Geard Ajetovic. Cheka anamkaribisha Ajetovic, Mwingereza mwenye asili ya Serbia, katika pambano hilo la raundi 12 uzito wa Super Middle, linalotazamwa kama marudiano ya mtifuano baina ya wawili hao waliowahi kuchapana jijini Manchester, Uingereza mwaka 2008. na Cheka kupoteza mpambano uho kwa point  Wawili hao wametambiana vya kutosha, kila mmoja akijinasibu kuwa yu tayari kumuadabisha mwenzake, Cheka akienda mbali zaidi kwa kusema hatarajii kuwaangusha Watanzania, hususani anapopigana katika ardhi ya nyumbani. Pambano hilo limeratibiwa na Kampuni za Advance Security kwa kushirikiana na Hall of Fame Boxing and Promotions zote za Dar es Salaam, ambalo litatanguliwa na mapambano mengine manne, ikiwamo burudani ya muziki kutoka kwa Bendi ya Twanga Pepeta. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa upimaji uzito, Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile, alisema maandalizi yote ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumsapoti Cheka. Ndambile, alisema viingilio vimegawanyika makundi mawili, ambako kiingilio cha juu kitakuwa ni Sh. 50,000 kwa Jukwaa la VIP, wakati cha chini ni Sh. 15,000 kwa viti vya kawaida. Aliyataja mapambano ya utangulizi kuwa kati ya Mohammed Matumla dhidi ya Mustapha Dotto (uzito wa Light raundi nane), Mohammed Bakari na Cosmas Cheka (Feather raundi nane) na lile la Lulu Kayage dhidi ya Mwanne Haji (Fly Raundi sita)a ajili ya
  mpambano wake


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...