Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 25, 2011

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LAZINDULIWA LEO


Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' (kulia) akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Sauti za Busara, Nahaat Mahfoudh wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha hilo, Dar es salaam jana katikati ni Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Sauti za Busara, Dar es salaam jana litakalofanyika mwanzoni
Februari 9-13.Juma Nature ni kati ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo, kushoto ni Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Nahaat Mahfoudh na Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said.

Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara,Yusuf Mahmoud akizungumza katika mkutano wa ufunguzi rasmi wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari asubuhi hii katika hoteli ya Southen Sun,jijini Dar.katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Simai Said na kulia ni Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.Meneja wa Tamasha la Sauti Za Busara,Stella Stephen akizungumza katika mkutano huo.wengine ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,Brian Karokola,Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti Za Busara,Yusuf Mahmoud,Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara,Simai Said na Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.
Baadhi ya Wanahabari na Wasanii walioshiriki katika mkutano huo.
Ankal akiwa na wadau wa Sauti Za Busara,toka shoto ni Yusuf Mahmoud,Waziri Ally, Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel pamoja na Simai Said.

Sauti za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litafanyika kwa mara ya nane visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia Februari 9-13.
Tamasha hili hukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisheherekea na kufahamiana kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la mwaka 2010.

“tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tamaduni mbalimbali kubadilishana mawazo,kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. Kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa tamaduni na urafiki.”

Sauti za Busara huwakutanisha wasanii wakubwa wa muziki barani Afrika pamoja na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni, Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin), Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band aka Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (South Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jagwa Music (Tanzania), Bismillahi Gargar (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Christine Salem (Reunion), Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), Jahazi Modern Taarab (Tanzania), Les Frères Sissoko (Senegal), Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East), Groove Lélé (Reunion), Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various), Djaaka (Mozambique), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band Namasabo (Tanzania), Lelelele Africa (Kenya), Atemi & the Ma3 Band (Kenya), Sauda (Tanzania).

Sherehe za mwaka huu zitafunguliwa na maonyesho mbalimbali ya kuvutia, muziki wenye nakshi mbalimbali ikiwemo nyimbo za kiswahili, madansa, maonyesho ya vipande vya filamu za muziki kutoka Tanzania, Uganda, DRC, Ivory Coast na Senegal.

Wakati huohuo, tamasha litadhamini Busara Xtra, yaani matukio ya nje ya tamasha yatakayoandaliwa ndani ya Zanzibar na ambayo yatawavutia na kuwanufaisha wageni waalikwa.
Hii itatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kuwahamasisha wageni kuendelea kutazama maeneo mengine ya visiwa na kuongeza kipato kwa watu wengi.
Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' (kulia) akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Nahaat Mahfoudh wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha hilo, Dar es salaam jana katikati ni Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said

Sunday, January 23, 2011

Super D kocha mwenye matarajio ya kuwafikisha vijana mbali katika ngumi


Awaomba wadau kushirikiana nae kuwasaidia vijana
MICHEZO hasa mchezo wa ngumi ni miongoni mwa michezo wenye msukumo mkubwa ukiwa umewapatia vijana nafasi ya kuwavutia katika jamii hasa katika kpindi hiki ambapo jamii zinajihusisha kwa karibu na michezo.

Ipo michezo katika jamii hasa hapa nchini ambayo imepokelewa kwa kiwango cha hali ya juu na mingine ikiwa bado haijapatiwa nafasi kubwa kama ambavyo inaonekana.

Mfano wa michezo ambayo imepta nafasi kubwa ya kupendwa na watu wengi hapa nchini ni mchezo wa mpira wa miguu, mchezo wa ngumi, na mchezo wa mchezo wa kikapu ingawa takwimu zinaoneshwa kuwa m,chezo wa kikapu ni wa pili kupendwa hapa nchini.

Ukiachilia mbali michezo hii ipo michezo mingine ambayo bado haijapewa nafasi kubwa katika maeneo mengi kwa mfano mchezo wa kriketi, gofu, mchezo wa meza, mpira wa mikono, tenisi na mingine mingi.

Wadau wengi wa michezo hapa nchini wamekuwa wakijihusisha karibu na michezo lakini wanashindwa kusonga mbele kutokana na msukumo wa jamii katika michezo kuwa mdogo inayopelekea kukosa wadau kudhamini michezo.

Kocha wa kujitegemea wa ngumi anayefundisha klabu ya Ashati ya Ilala Jijini Dar es Salaam Rajabu Mhamila 'Super D' ameanzisha programu maalumu ya kuwafundisha vijana anayoiendesha katika ufukwe wa bahari ya Hindi, sehemu ya Coco Beach.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii hivi karibuni jijini Dar es Salaam Super D alisema alisema ameamua kuanzisha ili kutumia vizuri kipaji chake alichopewa na wengine waweze kufaidika nacho nao waweze kufaidika nacho.

"Nimeona vijana wengi hawana kazi wapo tu mitaani na wanavipaji sasa nafundishwa kwa kujitolea ili kuibua vipaji vyao na hatimaye waweze kutimiza malengo yao katika maisha.," alisema Super D kocha wa ambaye aliwahi kuchezea klabu ya zamani ya ngumi ya Simba Boxing Jijini Dar es Salaa.

Super D ambaye kitaaluma ni mwandishi wa Habari na mpiga picha wa Magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Maisha, Dar Leo na Business Times yanayochapishwa na Kampuni ya Business Times ya Jijini Dar es Salaam anasema anaamini vijana wengi wanaweze kufika mbali kupitia mchezo huu kama wakiwezeshwa.

Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka hadi kufikia nane.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.
Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka hadi kufikia nane.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.
Anasema mabondia aliokuwa nao hadi hadi sasa wanafuatilia kwa makini mafunzo yake ambapo wengi wao wameonekana kuonesha nia na mapenzi ya dhati na mchezo huo.

"Sina shaka nao hata kidogo wanafanya vizuri na nawapongeza wanafuatlilia kwa makini na wananielewa viwango vyao vinazidi kubadilika kila kukicha wananipa moyo na nadhani watatimiza lengo.," anasema.

Akizungumzia mafanikio yake hadi amefanikiwa kuwa kocha Super D anasema alianza kujihusisha na mchezo wa ngumi mwaka 1984 na kujipatia uzoefu mkubwa baada ya kuchezea klabu mbalimbali za mchezo huo jijini Dar es Salaam.
Anasema klabu alizowahi kuchezea ni pamoja na klabu ya zamani ya Boxing iliyokuwa chini ya klabu ya soka ya Simba mwaka 1984, klabu ya reli iliyokuwa inamilikiwa na mamlaka ya reli kariakoo, pamoja na klabu ya Amana ya Ilala zote za Dar es Salaam.


Super D anasema akiwa bondia alipata nafasi ya kucheza na mabondia mbalimbali akiwemo Mbwana Matumla, Rashid Ally, Husein Pazzi, Alfred Ngaloma na bondia Roja Mtagwa ambaye ndiye bondia aliwewahi kumshinda kati ya hao ambaye kwa sasa anacheza ngumi nchini Marekani.
Alisema mabondia wengine aliowahi kucheza nao ni Oscar Manyuka, na Said Chaku ambaye kwa sasa ni mwamuzi wa mchezo huo katika mashindano mbalimbali yanayofanyika hapa nchini.
Hata hivyo hivi karibuni baada ya matunda ya kazi yake kuanza kuonekana kutokana na watu wengi kupendelea kupita na kutazama kazi yake baadhi ya wadau wameanza kujitokeza na kumpongeza.

Hata hivyo kocha huyo anasema anawaomba wadau wa mchezo huo wataungana naye kimsapoti ili kuwaendeleza vijana kutokana na ukosefu wa vifaa unaowakabili na wengi wao kushindwa kuhudhulia.

Anasema baada ya kuanza kazi yake hadi sasa amefanikiwa kumpata mdau mmoja aliyemtaja kwa jina la Zulfiqal Ali ambaye ameweza kumsapoti kwa kumpatia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi laki tatu.

"Ninamshukuru sana na nina mpongeza kwa kitendo chake cha kiungwana kuniunga mkono kuwasaidia vijana, nafikiri mfano wake utaigwa na wadau wengine namhakikishia ataifurahia kazi yangu,." anasema kocha huyo.

Hata hivyo kocha huyo amewataka wadau wengine kumuunga mkono katika kazi yake ambapo pia amewaomba wazazi kuwaruhusu vijana wao ambao wanavipaji kuhudhulia mazoezi yake ili kuendeleza vipaji vyao.

NMB YATOA MSAADA SHULE YA MONDULI JUU

Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale (kushoto) akikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi wa tanki la maji kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Monduli Juu, Elinuru Sumari (kulia). Wengine ni Meneja wa Benki tawi la Monduli.Asterina Mwigamba (wapili kushoto) na Ofisa Mikopo wa benki hiyo, Helga Nkini. Tanki hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita 600. Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo jana. (NA MPIGA PICHA WETU)

KAMANDA MWAIKENDA ACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA WANAFUNZI UDSM

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa Sh. 10,000 kutoka kwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuchangia ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Jakaya Kikwete alichangia jumla ya shilingi milioni kumi.(PICHA NA FREDDY MARO)

Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Wanafunzi uliofanyika ikulu jijini Dar es S alaam jana usiku.Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala. Shilingi bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Jakaya Kikwete alichangia Shilingi milioni kumi. (PICHA NA FREDDY MARO)

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group Tanzania Limited, Yussuf Manji (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau wakati wa hafla hiyo.

Gavana wa Benki Kuu (BOT), Profesa Beno Ndulu (kulia) akizungumza na Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Super Doll na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, Nassoro Seif (katikati) pamoja na Mmiliki wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited, Ghulam Dewji wakati wa hafla hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Injinia Prosper Tesha (kushoto), akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa kwenye harambee hiyo


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe walipokutana kwanye hafla hiyo.
Msereheshaji wa Harambee hiyo, Anjela Pondo, akimuonesha Rais Jakaya Kikwete jumla kuu ya fedha zilizochangwa.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wanamuziki wa Bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde' waliotumbuiza hafla ya uzinduzi wa kuchangia ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Jakaya Kikwete alichangia jumla ya shilingi milioni kumi.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

SHUJAA WA SAFARI LAGER AKABIZIWA MILIONI SABA


Kiongozi wa bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto akiimba wakati wa onesho lalo wakati wa kumsaka shujaa wa Safari Lager Dar es salaam juzi
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga akimkabidhi mshindi wa shindano la Shujaa wa Safari Lager Bw. Paul Luvinga mfano wa hundi ya shilingi milion saba Dar es salaam juzi wanaoshuudia kushoto ni Meneja wa bia hiyo Bw. Fimbo Butallah kushoto Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Bw.(Stive Kilindo na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw. Davidi Minja

Friday, January 21, 2011

LIFT YAKWAMA KATIKA JENGO LA MWALIMU HOUSE





Polisi wakiendelea na kuimalisha usalama katika jengo la Mwalimu House Ilala Dar es Salaam baada ya kukwama kwa lifti masaa manne ikiwa na watu ndani jana
Mmoja ya waliokolewa katika lifti ya gorofa ya Mwalimu House iliyopo Ilala Dar es salaam jana akipunga mkono juu kuashilia anashukulu kwa kutoka salama kwenye lifti hiyo iliyokwama kwa mda wa masaa manne

TRENI KUANZA KUONDOKA LEO


KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imerudisha huduma za usafiri wa reli ya kati baada ya kusimama kutokaa na uharibifu katika daraja la mto Bububu lililopo kati ya stesheni ya Bahi na Kitinku.

Uharibifu huo ulitokana na mafuriko ya maji yaliyokuwa yakipita katika mkondo wa mto huo na kusababisha nguzo moja kuharibiwa.

Mkuu wa usafiri wa Reri wa TRL BW.Charles Ndenge aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuwa safari hizo zimeanza leo saa 11 jioni kwa treni inayotoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.

"Uwamuzi wa kuanza tena huduma unatokana na kukamilika kwa kazi ya kukarabati daraja lililo katika ya stesheni ya Bahi na Kintinku ambalo nguzo yake moja iliharibiwa na kuondoka na maji ya mto Bububu unaoanzia wilayani Kondoa,Dodoma "alisema Bw.Ndenge

Bw.Ndenge alisema wakati huo huo treni ya abiria iliotoka juzi Kigoma kwenda Dar es Salaam imeshawasiri Tabora ambapo inatarajiwa kupita kaika daraja hilo saa 11:15 jioni.

Aliongeza kuwa huduma ya safari hizo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma utaendelea kuwa marambili kama ilivyotangazwa awali kwa siku za jumanne na Ijumaa.

Hata hivyo alisema kuwa safari za treni za kwenda Mwanza bado hazijaanza na wanaendelea kufanyia ufumbuzi suala hilo kwa kuanza na ukarabati mabehewa ya kubebea abilia watakaokwenda huko.

Tryphone mweji atunukiwa tuzo ya heshima

Mwandishi wa Habari Mkongwe wa kampuni ya the Guardian, Tryphone Blassius Mweji (katikati) akitunukiwa tuzo ya kuwa Mwanachama wa Heshima ya Kutukuka wa Klabu za Lions ( Lions club International honorary
member) kutoka kwa Gavana Wilson Tumwine wa Uganda, kwenye hafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Anayekabidhi tuzo hiyo kwa
niaba ya Gavana ni Mwwenyekiti wa Baraza la klabu za Lions za Uganda
na Tanzania, Safdar Jaffer

SAFARI YA SIMBA BRAZIL YAOTA MBAWA

Mabeki wa Simba Juma Jabu (kulia) na Haroon Shamte, wakishangilia bao lilillofungwa na Mussa Hassan mgosi kipindi cha kwanza baada ya Krosi nzuri iliyopigwa naye Juma Jabu.
Kiungo wa timu ya Simba, Jerry Santo (kushoto) akiruka kuwania mpira na beki wa Atletico Paranaense ya Brazir, Patrick Leonaldo, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam

YANGA VURUGU TUPU

Viongozi wa Matawi wakiwa tayari kwa Mkutano
Wakianza Mkutano kwa Dua
Dua..
Mwenyekiti, Mohamed Msumi akifungua kikao
Msumi akizungumza
Msumi akiendelea kuzungumza na Viongozi wa Matawi
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yannga akijibu swali juu ya Mkataba wa Kocha Papic
Wajumbe wakifuatilia kwa makini
Mpaka kieleweke
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...