Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 21, 2011

TRENI KUANZA KUONDOKA LEO


KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imerudisha huduma za usafiri wa reli ya kati baada ya kusimama kutokaa na uharibifu katika daraja la mto Bububu lililopo kati ya stesheni ya Bahi na Kitinku.

Uharibifu huo ulitokana na mafuriko ya maji yaliyokuwa yakipita katika mkondo wa mto huo na kusababisha nguzo moja kuharibiwa.

Mkuu wa usafiri wa Reri wa TRL BW.Charles Ndenge aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuwa safari hizo zimeanza leo saa 11 jioni kwa treni inayotoka Dar es Salaam kwenda Kigoma.

"Uwamuzi wa kuanza tena huduma unatokana na kukamilika kwa kazi ya kukarabati daraja lililo katika ya stesheni ya Bahi na Kintinku ambalo nguzo yake moja iliharibiwa na kuondoka na maji ya mto Bububu unaoanzia wilayani Kondoa,Dodoma "alisema Bw.Ndenge

Bw.Ndenge alisema wakati huo huo treni ya abiria iliotoka juzi Kigoma kwenda Dar es Salaam imeshawasiri Tabora ambapo inatarajiwa kupita kaika daraja hilo saa 11:15 jioni.

Aliongeza kuwa huduma ya safari hizo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma utaendelea kuwa marambili kama ilivyotangazwa awali kwa siku za jumanne na Ijumaa.

Hata hivyo alisema kuwa safari za treni za kwenda Mwanza bado hazijaanza na wanaendelea kufanyia ufumbuzi suala hilo kwa kuanza na ukarabati mabehewa ya kubebea abilia watakaokwenda huko.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...