Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 11, 2011

RUVU SHOOTING MABINGWA UHAI CUP

Timu ya RUVU SHOOTING baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la vijana wakati wa michuano iliyokuwa inafanyika kwenye uwanja wa KARUME Jijini DSM
Baada ya kupokea kikombe wachezaji wa timu ya RUVU SHOOTING wakifurahi
Nahodha wa RUVU SHOOTING akikabidhiwa kikombe na Mkurugenzi wa Idara ya michezo LEONARD THADEO Jijini DSM
Rais wa TFF LEODGER TENGA akimkabidhi zawadi mwamuzi bora
Baada ya mchezo kumalizika wachezaji wa RUVU SHOOTING wakipumzika
Kushoto Katibu mkuu wa TFF OSEAH pamoja na mkurugenzi wa masoko TFF JIMY KABWE wakiangalia kwa makini fainali za kombe la vijana kati ya RUVU SHOOTING na JKT RUVU
Mdhamini wa mashindano haya akikabidhi medali kwa wachezaji wa timu ya JKT RUVU baada kushika nafasi ya pili
MWASAMAKI akikabidhiwa medali na mwenyekiti wa mashindano hayo MSAFIRI MGOI wakati wa fainali hizo
Waamuzi waliofanikisha mashindano ya uhai wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi wakati wa kufunga mashindano ya vijana katika uwanja wa KARUME Jijini DSM.

Timu ya RUVU SHOOTING imefanikiwa kutwaa kombe la vijana chini ya miaka ishirini baada ya kuifunga timu ya JKT RUVU magoli mawili kwa moja katika fainali zilizofanyika uwanja wa KARUME Jijini DSM,RUVU SHOOTING wametwaa kombe hilo na kujinyakulia kititat cha shilingi milioni moja na nusu,wakati mshindi wa pili milioni moja ambao ni JKT RUVU na mshindi wa tatu ambao ni AFC ARUSHA wamejinyakulia shilingi laki tano NA http://janejohn5.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...