Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 17, 2011

PROMOSHENI YA HAMIS MA SMS YAFIKIA TAMATI

Hamisi ma SMS mwezeshaji wa promosheni ya Zantel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kufikia mwisho wa promosheni hiyo iliyoendeshwa kwa takribani miezi 3 na kuwafanya wateja 109 kuwa mamilionea . Wakimsikiliza ni William Mpinga (kushoto) Mkuu wa Mahusiano Zantel na Brian Karokola (wa pili kushoto) Kaimu Mkurugenzi Masoko Zantel.

Kampuni ya Simu za mkononi ya Zantel leo imechezesha droo kubwa na ya mwisho ya promosheni yake maarufu ya Hamisi ma SMS. Droo ilichezeshwa na Hamisi ma SMS aka Mzee wa Kutoa Cheda mwenyewe ikisimamiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya bahati nasibu nchini. Bi. Wazire Mustafa Abdallah ndiye aliyeibuka mshindi wa milioni 15 na kuwa mshindi wa mwisho wa promosheni ya Hamisi ma SMS iliyofikia tamati Jumapili tarehe 9 Januari 2011.

Promosheni ya “Hamisi ma SMS” iliendeshwa kwa muda wa siku 98 na ilikuwa ikitoa zawadi ya milioni 1 kwa mshindi mmoja kila siku, milioni nyingine moja kila wiki kwa mteja aliyetuma meseji nyingi kila wiki na milioni 15 kila mwezi. Promosheni ya Hamisi ma SMS imefanikiwa kuwafanya wateja 109 wa Zantel kuwa mamilionea na kutumia jumla ya milioni 151 kama zawadi kwa washindi.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuendesha droo ya mwisho ya promosheni hii, Brian Karokola, Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Zantel alisema nia na madhumuni ya kuanzisha promosheni ya Hamisi ma SMS ilikuwa ni kuwatuza wateja wa Zantel kwa upendeleo wao na uaminifu kwa Zantel. “Sisi kama Zantel tunajivunia mafanikio tuliyoyapata kupitia promosheni hii na tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba tunatambua na kuthamini ushirikiano wao. Hamisi ma SMS sasa amekuwa mtu maarufu sana na amefanikiwa kupata wafuasi wengi kwa sababu ya ucheshi na ukarimu wake.” alielezea Bw. Karokola.

Kwa upande wake Hamisi ma SMS pia aliwashukuru wateja wa Zantel kwa ushirikiano wao kipindi chote cha promosheni na kuahidi kurudi tena kwa kishindo. “Nilipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini kukutana na wateja wa Zantel pamoja na kugawa laini za simu kwa wateja wapya na kutoa misaada kwenye vituo mbalimbali vya wazee na watoto yatima. Mwisho wa promosheni ya Hamisi ma SMS ni mwanzo wa kitu kingine kipya.” alisisitiza Bw. Hamisi ma SMS.

Mwezeshaji wa promosheni ya Hamisi ma SMS Nixon Haule (katikati) akibonyeza kitufe kuchezesha droo ya mwisho kumpata mshindi wa milioni 15 iliyofanyika katika ofisi za Zantel mwishoni mwa wiki iliyopita na Bi Wazire M. Abdalla mkazi wa Malindi Zanzibar aliibuka mshindi. Wengine pichani ni Brian Karokola Kaimu Mkurugenzi Masoko Zantel (Kushoto) na Abdallah Hemedy Afisa kutoka bodi ya michezo ya bahati nasibu.

Mkuu wa Mahusiano Zantel William Mpinga akizungumza kwenye simu na mshindi wa milioni 15 kwenye droo ya mwisho ya promosheni ya Hamisi ma SMS Wazire M. Abdalla mkazi wa Malindi Zanzibar iliyofanyika makoa makuu ya Zantel Dar es Salaam. Wengine kwenye picha ni Brian Karokola (wa tatu kulia) Kaimu Mkurugenzi Masoko Zantel, Hamisi ma SMS na Abdalla Hemedy Afisa kutoka bodi ya michezo ya bahati nasibu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...