Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 4, 2011

ASHANTI BOXING WATAJA MABONDIA WAKE


Klabu ya Ngumi ya Ashanti yateua mabondia sita mashindano ya mkoa Ilala

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya ndondi ya Ashanti imetaja majina ya mabondia sita watakaoiwakilisha klabu hiyo kwenye mashindano ya mkoa wa Ilala yanayotarajia kuanza januari 8 mwaka huu katika ukumbi wa Ndadu Pub Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Kocha wa klabu hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema mabondia waliowachagua wana uzito tofauti tofauti na wana uzoefu mkubwa katika mchezo huo.

Aliwataja mabondia hao kuwa Miambo Mussa, Msami hatibu, Ramadhani Kimangale (kilogramu 60), Nasri Ali(kilogramu 58), Mark Edie (Kilogramu 50) na Raymond Robert (Kilogramu 50)ambao aliwaelezea kuwa wana uwezo mkubwa.

"Mabondia hawa wamejifunza katika klabu yetu na wana uzoefu mkubwa sana tangu walipoanza, tuna matumaini makubwa watafanya vizuri na kuitangaza klabu yetu katika nyanja za juu.," alisema Mhamila.

Super D aliongeza kuwa kutokana na uwezo walionao mabondia wake watafanya vizuri zaidi ya uwezo wao na kuongeza kuwa upo uwezekano mkubwa wa mabondia wote kuchaguliwa kuiwakilisha Wilaya hiyo kama mkoa kushiriki mashindano ya Taifa.

Katika hatua nyingine Super D ametoa wito kwa wadau na wapenzi mbalimbali wa mchezo wa ngumi kuidhamini timu yao katika mashindano hayo.

Mbali na klabu ya Ashanti klabu zingine zitakazoshiriki mashindano hayo ni Amana, Mtakuja, na Simba za wilaya ya Ilala.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...