Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 8, 2011

MBUNIFU WA VITU MBALIMBALI

Bw.Salum Athumani (43) maeneo ya katikati ya jiji akiwa amezungukwa na umati wa watu wakishangaa ubunifu na kipaji kikubwa alichonacho.

Bw. Salum mkazi wa Tandika Azimio mwenye elimu ya darasa la 7 amevutia macho ya wengi ikiwemo kamera ya MO BLOG kwa kubuni vifaa mbalimbali kwa kutumia miti pamoja plastiki, rangi kutengeneza mifano ya greda, nyumba, kifaru, na vinginevyo.

Salum amesema ametumia muda wa miezi sita (6) kutengeneza vitu hivi vyote kwa msaada wa ndugu yake wa karibu ambaye anaishi naye maeneo ya Tandika.

Aidha mbunifu huyo ameiomba Serikali iwaangaalie watu kama yeye wenye upeo na vipaji vikubwa vya kuweza kubuni na kuunda vitu kama hivyo.

Lengo lake kubwa kubuni vitu hivyo ni ili serikali iweze kuona umuhimu wa kuwatambua na kuwawezesha watu kama yeye, akiamini wakisaidiwa wanaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya hayo.

MO BLOG inachukua fursa hii kumpongeza Salum Athuman kwa uwezo na uthubutu wake wa kuonyesha ubunifu kama huo. Pia inaamini wako watu wengi wenye uwezo kama huo ambao wakitumiwa vizuri na kuendelezwa kielimu wanaweza kubadilisha taswira ya teknolojia hapa nchini.

Zinazofuata ni picha zinazoonyesha baadhi ya vitu alivyobuni Bw.Salum Athuman

Bw. Salum Othman akionesha jinsi ya ufanyaji kazi wa vifaa hivyo alivyobuni mfano wa Greda ambalo amebuni.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...