Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 6, 2011

DAMU YA CHADEMA ILIVYOMWAGIKA JANA

Viongozi wa CHADEMA katika maandamano leo kabla ya kutawanywa na polisi na wengine kutiwa mbaroni
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa mji wa Arusha wakiwa wameshika mabango katika maandamano hayo kabla ya wanausalama kuanza kuzuia maandanayo hayo.
Huyu Dogo balaa pia nae alikuwepo katika maandamano hayo,ambapo naamini kabisa kwamba aliingia katika maandamano hayo kwa kufuata mkumbo tu.maana umri wake unaonekana ni mdogo sana.
Mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr. Willbroad Slaa.Mama Josephine Kamili akichuruzika damu mara baada ya kutokea kwa vurugu baina ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA dhidi ya Askari Polisi.Vurugu hizo zimezuka mchana wa leo huko mkoani Arusha mara baada ya kuzuiliwa kufanya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa na chama hicho.
Askari Polisi wakijaribu kulizuia gari moja lilikuwepo katika maandamano hayo.
Wanausalama wakimtuliza mmoja wa waandamanaji aliekuwepo katika maandamano hayo.
Wakazi wa maeneo ya jirani na zilipotokea vurugu hizo wakinawa maji usoni ili kupunguza makali ya sumu za mabomu ya machozi yaliyokuwa yakilipuliwa katika kutuliza ghasia hizo.
Mitaa ya Jijini Arusha ililindima milio ya Mabomu ya Machozi huku mitaa ikiwa imepoa kabisa.
Askari Polisi wakiwa wameenea kila kona kuhakikisha hali inakuwa shwari na hakuna mtu anaefanya maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...