Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 19, 2011

YANGA YAFUNGWA NA Timu ya Altetico KUIONA SIMBA KESHO BULEE

Timu ya Altetico Paranaense ikiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous kabla ya kuelekea uwanjani kwa mchezo dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji wa timu ya Atletico Paranaense,Gabriel Lima De Oliveira akijaribu kumtoka kipa wa Yanga,Nelson Kimath wakati wa mcheo wao wa kirafiki uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa.timu ya Atletico Paranaense imeshinda 3-2 dhidi ya Yanga.
Beki wa Atletico Paranaense,Diego Alexandre Petri akichuana vikali na kiungo wa timu ya Yanga,Abuu Zubeir katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa.timu ya Atletico Paranaense imeshinda 3-2 dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji wa Yanga,Nsa Job akiwa na mpira kuelekea langoni mwa timu ya Atletico Paranaense huku beki wa timu hiyo,Diego Alexandre Petri akimkimbiza ili kuondoa hatari hiyo.
Davis Mware wa Yanga akijaribu kumtoka beki wa timu ya Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa.timu ya Atletico Paranaense imeshinda 3-2 dhidi ya Yanga.
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu ya Yanga ya jijini na Atletico Paranaense ya nchini Brazil uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar leo.Mama Rahma Al - Kharous amewataka watanzanzia kujitokeza kwa wingi katika mchezo unaofuata dhidi Simba ya jijini na timu hiyo ya kigeni utakaochezwa kesho kutwa uwanjani hapo,pia amesema kuwa hakutakuwa na kiingilio siku hicho watanzania tujitokeze kwa wingi kuisapoti timu hiyo.
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous akiwa na viongozi wa timu ya Atletico Paranaense wakiwa wameshikilia bendera za mataifa mawili ikiwa ni ishara ya umoja katika michezo.http://issamichuzi.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...