Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 27, 2011

AIRTEL YAWAKUMBUKA WANA HABARI


KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel imeandaa bonanza litakaloshirikisha vyombo mbalimbali vya Habari ambalo limepangwa kufanyika Februari 12 mwaka huu katika viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama, Dar es Salaam.

Bonanza hilolinatarajiwa kushirikisha wanahabari zaidi ya 500 kutoka katika vyombo arobaini hapa nchini likihusisha michezo mbalimbli.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano alisema lengo la bonanza hilo ambalo wanalianda kila mwaka ni kuimarisha ushirikiano baina yao na vyombo vya Habari na kuendelezamahusiano.

"Ni kawaida katika kila mwisho au mwanzo wa mwaka kufanya tathimini ya jumla ya pale tulipo na wapi tunakwenda na pia tunakitumia kipindi hikikukaa na kufurahi pamoja na watu wenye majukumu tofauti miongoni mwao ni nyinyi wanahabari.," alisema Mkuu huyo.

Alisema michezo ambayo itachezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu utakaohusisha timu zawatu saba kutoka kila upande, kukimbia kwa magunia, kuvuta kamba, kushindana kunywa soda, na mingine mingiambapo zawadi mbalimbali zikiwemo vikombe zitashindaniwa na vyombo hivyo na washiriki binafsi.

Beatrice alisema bonanza hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi ya msimu uliyopita na kwamba kutakuwa burudani kutoka kwa bendi ya muziki waambayo itatangazwa baadae.

Hata hivyo alisema wataendelea kutoa taarifa za jinsi wanavyoendelea na taratibu za maandalizi ambapo pia wanakaribisha maoni kutoka katika vyombo vya habari kuelekea katika bonanza hilo.

Naye Mratibu wa Tamasha hilo na mwakirishi wa Kampuni ya Capital-Plus International ambao ndio waratibu, Mawazo Waziri alisema alisema maandalizi yanaendelea kufanyika kwa mafanikio makubwa na kuongeza kuwa kutakuwana mashindano ya kuimba na kucheza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...