Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 23, 2011

KAMANDA MWAIKENDA ACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA WANAFUNZI UDSM

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa Sh. 10,000 kutoka kwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuchangia ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Jakaya Kikwete alichangia jumla ya shilingi milioni kumi.(PICHA NA FREDDY MARO)

Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Wanafunzi uliofanyika ikulu jijini Dar es S alaam jana usiku.Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala. Shilingi bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Jakaya Kikwete alichangia Shilingi milioni kumi. (PICHA NA FREDDY MARO)

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo (katikati) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group Tanzania Limited, Yussuf Manji (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau wakati wa hafla hiyo.

Gavana wa Benki Kuu (BOT), Profesa Beno Ndulu (kulia) akizungumza na Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Super Doll na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, Nassoro Seif (katikati) pamoja na Mmiliki wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited, Ghulam Dewji wakati wa hafla hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Injinia Prosper Tesha (kushoto), akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa kwenye harambee hiyo


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe walipokutana kwanye hafla hiyo.
Msereheshaji wa Harambee hiyo, Anjela Pondo, akimuonesha Rais Jakaya Kikwete jumla kuu ya fedha zilizochangwa.

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wanamuziki wa Bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde' waliotumbuiza hafla ya uzinduzi wa kuchangia ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zilikusanywa katika hafla hiyo ya uzinduzi ambapo Rais Jakaya Kikwete alichangia jumla ya shilingi milioni kumi.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...