Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 19, 2011

Azania Benki ya Sherehe ya mwaka mpya


Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Azania imelenga kupanua huduma zake katika mwaka huu kwa kufungua
matawi katika maeneo ya Mbezi Mwisho Kariakoo, Sam Nujoma, Dar es salaam,
Katoro/Biharamulo, Arusha, Lamadi/Simiyu, Kogongwa/Kahama, Geita na Tunduma.
Hatua hii ni mkakati wa kimaendeleo wa benki hiyo katika kujiimarisha kihuduma
kwa kuwafikia wateja wengi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba
wamefikia hapo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya
menejimenti,wamiliki,wafanyakazi na wateja wa benki hiyo kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Singili aliyasema hayo katika hafla
yakuukaribisha mwaka mpya iliyofanywa na benki hiyo katika Kisiwa cha Bongoyo
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Singili alisema benki hiyo inaendelea na mikakati kuhakikisha kuwa huduma zao
zinaendelea

kuimarika kadri miaka inavyosonga mbele na kwamba uongozi unawashukuru wadau
wote wa kibenki waliowawezeshsa kufika hapo walipo..
Kwa upande mwingine alitoa shukrani za pekee kwa wamiliki wa benki hiyo (NSSF,
PPF, PSPF,

LAPF, EADB) ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa benki hiyo inakua na
kuwa imara

wakati wote ambapo alitoa rai kwao pamoja na wadau wengine kuongeza bidii ili
benki hiyo iweze kupiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo mwaka huu.

“Mafanikio tuliyofikia ni matokeo ya kazi nzuri ya menejimenti ya benki pamoja
na wadau mbalimbali wa kibenki wakiwemo wateja wanaounga mkono huduma zetu hivyo
tunatoa shukrani kwa jamii nzima ya kitanzania wakiwemo wamiliki wetu kwa
kuifanya Azania isonge mbele,” alisema.
Aliongeza kuwa pamoja na maeneo hayo pia benki hiyo ina mpango wa kufungua
matawi mengine

katika mikoa ya Dodoma,Morogoro na Mbeya na kwamba upanuzi huu wa huduma
utakwenda kwa awamu kulingana na uwezo wa kifedha wa benki.
“Kiukweli tumedhamiria kuendelea kujiimarisha na mpango wetu umelenga zaidi
kupanua huduma

ili kuwafikia watanzania wengi zaidi, tumepanga kufika kila kona ya nchi na
kwamba hilo litaangalia uwezo wetu wa kifedha lakini ni matumaini yetu kuwa
malengo yetu yatatimia,” alisema Singili.
Wamiliki Wazalendo wa Benki ya Azania wanayoisimamia kwa miaka kumi ya
kujiendesha na kiasi

cha hisa wanazomiliki ni NSSF 35%, PPF 30%, PSPF 12%,LAPF 14%, EADB 6% wakati
wadau wengine

wa kawaida wa kitanzania na wafanyakazi wa benki hiyo wanamiliki 3% ya hisa za
jumla za benki hiyo.

Kwa sasa benki hiyo ina mtaji wa sh. bilioni 19/- na wakmba tayari imefungua
matawi saba katika maeneo mbalimbali nchini katika miaka kumi ya kujiendesha
tangu ilipoanzishwa rasmi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...