Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 2, 2011

ZANTEL KUSAIDIA KITUO CHA KIDS CARE BAGAMOYO KWA MWAKA HUU


KAMPUNI ya simu za mkononi Zantel imefungua mwaka kwa kula chakula na watoto yatima Kids Care cha Bagamoyo huku ikitoa ahadi mbalimbali kusaidia kituo hicho.

Akizungumza wakati wa mlo huo uliondaliwa maalumu kwa ajili ya watoto hao,Kaimu Mkurugenzi wa masoko wa kampuni hiyo,Bw.Brayani Kalokola alisema mbali na kula nao katika siku ya kwanza ya mwaka huu watasaidia kuendeleza kitu hicho kuwa saidia mahitaji yao.


Bw.Kalokola alisema kuwa mbali na kampuni wakampuni hiyo,wafanyakazi nao wapo tayari kujitolea kukisaidia kituo hicho kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani chenye mahitaji mbalimbali.

"Ningependa kutoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia yatima kwani wana mahitaji mengi,"alisema Bw.Kalokola.

Alisema kuwa endapo wadau mbalimbali watajitokeza kuwasaidia yatima watawawezesha kujikwamua katika matatizo mbalimbali yanayowakabili.

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...