Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 6, 2011

KAMPUNI YA ZANTEL YAGAWA VYANDARUA


KAMPUNI ya simu za mkononi Zantel imefungua mwaka kwa kugawa Vyandarua katika hospital ya Mwananyamala Dar es salaam leo.

Akizungumza wakati wa kugawa vyandarua hivyo kwa ajili ya kupambana na malalia, Mataalamu wa bidhaa wa kampuni hiyo Bw.Deogratius Ringia alisema mbali ya kutoa msaada huo wamejipanga kusaidia watu wenye maitaji maalumu kwa mwaka 2011.


Bw.Ringia alisema kuwa wametoa neti 100 zenye thamani ya shilingi laki tano kwa ajili ya wagojwa watakaokuwa hapo ili wasin'gatwe na mmbu.


"Ningependa kutoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kujitokeza kusaidia hospital mbalimbali kwani zina mahitaji mengi,"alisema Bw.Ringia.

Alisema kuwa endapo wadau mbalimbali watajitokeza kuwasaidia tatizo la malalia litatokomezwa kabisa nchini na litabaki historia.

Nae Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo Dkt.Ngonyani Sophinias ' amesema wamepokea msaada huo na vitatumika kama ilivyopangwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...