Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 10, 2012

SERIKALI YAAGIZA SUKARI KUTOKA NJE ILI KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI



 
SERIKALI imeagiza sukari Tani 29,1900 kutoka nje ya nchi  lengo likiwa ni  kushusha mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali nchini kwa asilimia 17.4.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa Baraza Jipya la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, Waziri wa sekta hiyo, Dk William Mgimwa alitabanaisha kwamba kutokana na utafiti uliofanywa na serikali kwa mwezi Julai  umebaini ongezeko la  asilimia 24.7  la bidhaa mbalimbali.
 
Alisema baadhi ya  bidhaa kama Sukari, Unga, na Mchele, zimeonekana zikipanda bei kwa kasi jambo ambalo linaashiria kuwaumiza walaji sambamba na kudumaza uchumi wa nchi.
 
“Vyakula vipo nchini, ila tatizo kubwa ni miundombinu kutokana na baadhi ya maeneo kuwa chakavu na kusababisha mazao kushindwa kufika sokoni kwa wakati au kufika kwa gharama kubwa” aliongeza Dk. Mgimwa.
 
Sambamba na hilo serikali imetenga dola  sh milioni 600 sawa na shilingi bilioni 93 kwa ajili ya mradi wa kuzalisha gesi, itakayosaidia usindikaji wa  bidhaa viwandani sambamba na ajira.
 
Alifafanua kuwa gesi hiyo itakuwa na uwezo wa kuzalisha megabaitsi 2000  jijini Dar es Salaam, na kusambazwa katika viwanda, Kampuni, Taasisi pamoja na  sekta muhimu mbalimbali zinazozalisha uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...