Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 10, 2012

CHAMA CHA WALIMU CWT CHATOA TAMKO LAKE KWA SERIKALI


 Rais wa Chama Cha walimu Tanzania Bw. Gratian Mukoba (Kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam kuhusiana na Tamko lao  kwa serikali kutaka iwarudishie madaraka wakuu wote waliovuliwa nyadhifa zao kwakuwa ni viongozi wa (CWT) ndio waliohamasisha mgomo. 
Vilevile chama hicho kimeitaka serikali  kufuta nia yake ya kuwashitaki walimu zaidi ya 180,000 walioshiriki mgomo kati ya walimu 233,440 walioko nchini kwani kwa kufanya hivyo watoto wa maskini wanaotegemea walimu hao kufundisha watakosa haki yao ya kufundishwa.Kulia na Kaimu katibu mkuu wa chama hicho Bw, Ezekiel Olotu.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
)Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Chama cha walimu CWT nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...