Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 10, 2012

USAIN BOLT ALIPOANDIKA HISTORIA MPYA MASHINDANO YA OLIMPIKI 2012


Bolt akimaliza kinara mita 200 akifuatiwa na Yohane Blake hayupo pichani na Warren Weir nyuma aliyeshika nafasi ya tatu
Usain Bolt kulia akipongezana na rafiki yake Yohane Blake baada ya kumaliza mbio za mita 200
Usain Bolt kushoto akiwa na mshindi wa pili Yohane Blake

LONDON, England

BINADAMU mwenye rekodi ya kasi duniani, Usain Bolt ameweka rekodi ya kuwa mkimbiaji wa kwanza kutwaa medali za dhahabu kwenye mbio za mita 100 na 200 za mashindano ya Olimpiki mara mbili mfululizo.
Bolt ameweka rekodi hiyo jana usiku, siku nne baada ya kutetea dhahabu ya mita 100, ambapo juzi alikimbia kwa sekunde 19.32 kumuwezesha kutetea dhahabu ya mita 200 akifuatiwa na Wajamaica wenzake Yohan Blake na Warren Weir.
Blake alikimbia umbali huo akitumia sekunde 19.44, huku Weir akikimbia kwa sekunde 19.88, wote wakiwa na miaka 22 mitatu nyuma ya Bolt.
Katika fainali ya mbio za mita 100 Agosti 5, Bolt aliyeonekana kama kushuka kiwango, alimfunika Blake kwa sekunde 9.63, aliyemgalagaza mkali huyo katika mbio za majaribio kupata wawakilishi wa Jamaica mwezi uliopita.
Bolt sasa ameifikia rekodi ya dunia iliyowekwa na Michael Johnson katika michezo ya Atlanta nchini Marekani mwaka 1996, ambapo kwa ushindi wake, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amepata heshima kubwa aliyokuwa akiiwania.
Baada ya kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 200, Bolt kama kawaida yake alishangilia kwa kufunga mikono kana kwamba anasali, kusujudu ardhini, kunyoosha kidole mbele na juu na kuonesha ishara ya kufyatua mshale kutoka kwenye upinde.
“Hiki ndicho ilikuwa nakitafuta na nimekipata. Najivunia sana hatua hii. Nilikuwa na msimu mbaya lakini nikaja hapa na kufanya nilichotakiwa kufanya” alisema akihojiwa na BBC.
“Tumekuwa tukijitahidi msimu wote, tulipeana moyo na hata kuweka shinikizo ili tufanikiwe, na sasa tunayo furaha,” alisema akijumuisha Wajamaica wenzake aliokuwa nao kwenye kambi ya timu ya nchi yao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...