Robin van Persie kushoto na Wayne Rooney kulia
Robin van Persie akishikilia tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England
Robin van Pesrie kushoto akisalimiana na Wayne Rooney katika moja ya mechi kati ya Arsenal na Man United
LONDON, England
MSHAMBULIAJI mahiri wa kimataifa wa
England, Wayne Rooney, ametoa mwito kwa Mholanzi Robin van Persie
kuungana naye klabuni Old Trafford yaliko makazi ya Manchester United.
Bosi
wa Mashetani Wekundu hao, Mskochi Sir Alex Ferguson, anahaha kupata
saini ya Van Persie nahodha na mshambuliaji tegemeo wa Arsenal kwa dau
la pauni mil. 20, huku Gunners ikionekana dhahiri kumbania.
Washika
Bunduki chini ya Mfaransa Arsene Wenger wameonesha kutokuwa tayari
kumuuza RVP kwa mahasimu wao wa Ligi Kuu ya England, ingawa United mara
kadhaa imetoa msisitizo wa kumuhitaji na kutaka kuwapo kwa mazungumzo.
Rooney
anayetamani kuunda pacha na Van Persie katika safu ya mbele ya Man
United, alisema: “Bila shaka, yeye ni mchezaji ninayevutiwa naye.
Amekuwa na kiwango cha kustaajabisha nakuvutia akiwa Arsenal kwa miaka
kadhaa sasa.
“Msimu uliopita unaweza kuwa
ndio bora zaidi kwake, kwani alifunga mabao mengi. Kama atakuja hapa,
anaweza kuwa na mchango mkubwa kwa kikosi na mafanikio makubwa.”
Alipoulizwa
kama angependa kufanya kazi pamoja na RVP katika safu ya mbele United,
Rooney alitabasamu na kujibu: “Ningependa kufikiria hivyo, lakini
unapaswa kumuuliza kocha juu ya hilo.
“Kuna
fowadi wengi hapa ambao wanacheza nami ama nafasi yangu, kuna Welbeck
(Danny), Chicharito na Berbatov (Dimitar) bado yuko hapa pia. Hivyo kuna
washambuliaji kibao wanaopigania nafasi hapa,” alimaliza Rooney.
Van
Persie amekana kurefusha mkataba wake Emirates akidaiwa kukimbia njaa
ya mataji kwa misimu saba sasa na Rooney anabainisha kuwa lengo kuu la
klabu yake ni kurejesha taji lililotwaliwa na majirani zao Manchester
City katika siku ya mwisho ya msimu.
No comments:
Post a Comment