Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Machinga
Complex, Bw. Abdubakar Rakesh akizungumza katika uzinduzi wa
utakaowawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga
complex jijini Dar es Salaam. Mpango huo utawawezesha wamachinga hao
kupata mikopo nafuu kwa ajili ua kuendesha na kukuza biashara zao ambapo
benki ya Equity kwa kupitia huduma ya Airtel Money na wao kuwa
wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel Money.
Mkurugenzi wa kampuni ya Ear Promotion ambao
wanasimamia na kuratibu mradi huo, Bw. Brian Kikoti aliwasifu benki ya
Equity pamoja na Airtel kwa kuungana nao katika kusaidia kusimamia
ufanisi wa soko la wafanyabiashara wadogo wadogo.
Umati wa watu waliohudhuria katika uzinduzi wa
utakaowawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga
complex jijini Dar es Salaam.
Bi. Sara Yohana aliyemwakilisha mkurugenzi wa jiji la
Dar es Salaam akisoma risala katika uzinduzi wa utakaowawezesha
wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es
Salaam.
Meneja Mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema
kuwa wataendelea na mikakati ya kusaidia jamii Nyanja mbali mbali za
kimaendelea kwa kupitia huduma ya Airtel Money katika mradi wa
upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi.
Dar es Salaam
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Equity bank
pamoja na Kampuni ya Ear promotion mwishoni mwa wiki hii imezindua mradi
utakaowawezesha
wafanya biashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar
es saalam kupata mikopo nafuu kwaajili ya kuendesha na kukuza biashara
zao ambapo mikopo hiyo itatolewa na benki Equity kwa kupitia huduma ya
Airtel money na wao kuwa wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia
Airtel money
Akizungumza
wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi huo, Meneja uendeshaji wa benki ya
Equity bw, David Mukaru alisema” equity benki iko mstari wa mbele
kuisaidia jamii katika huduma za kibenki ikiwemo mikopo ya riba nafuu
hasa akina mama wa vikundi mbalimbali.
Benki
yetu imekuwa sehemu ya maendeleo ya kukuza biashara na mtaji wa
wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa nchini. Leo kwa kushirikiana na
Airtel kupitia huduma ya Airtel money tunawawezesha wafanyabiasha wa
soko hili la machinga complex zaidi ya efu tano kupata mikopo ya riba
nafuu ambayo kwa hakika itakuza mitaji na kuwapatia ufanisi zaidi katika
biashara zao”.
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando
alisema ”Airtel tunaendelea na mikakati yetu ya kusaidia jamii katika
Nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwa kupitia huduma ya Airtel money,
katika mradi hu Airtel tunarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha
kupitia simu yako ya mkononi, tunawawezesha wafanyabiashara hawa kupokea
na kufanya marejesho ya mikopo yao kwa kupitia huduma ya Airtel money”
“lengo
letu Airtel ni kurahisi uendeshaji wa mikopo hii, kuhakikisha usalama
wa fedha, na kupunguza usumbufu wa wafanyabiashara hawa kutembea umbali
mrefu kufanya marejesho ya mikopo hii”. aliongeza Mmbando.
Naye mwenyekiti wa wafanyabisahara wa soko la machinga complex bw. Abdubakar Rakesh alisema ”ninaishukuru kampuni
ya Airtel pamoja na Equity benki kwa kutufikia sisi wafanya biashara
wadogowadogo kwa kupitia mradi huu wa mikopo nafuu. ni kwa muda mrefu
wafanyabiashara wa soko la machinga complex wamekuwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kupata mikopo nafuu ambayo itawawezesha kukuza mitaji
na kuweka bidhaa mbalimbali zitakazo wavutia wateja kufanya manunuzi
katika soko hili, hivyo kwa kupitia mradi huu tunaamini tutafanikisha
matarajio yetu ya kuwa na soko la kisasa lenye miundo mbinu na hadhi kwa
wafanyabishara na wateja wetu.
Naye
bw, Brian Kikoti Mkurugenzi wa Ear promotion Kampuni inayosimamia na
kuratibu mradi huo amewasifu Equity Benki pamoja na Airtel kwa kuungana
nao katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko hilo na la wafanyabiashara
wadogowadogo.
Mbali
na ushirikiano huu wa kibiashara na Equity bank, Airtel tayari
inashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo GEPF , LAPF, DAWASCO,
TANESCO, USA EMBASSY, COCACOLA na mengine mengi katika kutoa huduma zao
kupitia huduma ya Airtel money.
No comments:
Post a Comment