Tiketi
kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3
mwaka huu) zitaanza kuuzwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye vituo
mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili
usiku.
Vituo
vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya
Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom
Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala
na Kituo cha Mafuta Buguruni.
Kiingilio
cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani
ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni
17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
Sh.
10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C
inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B
tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa
sh. 30,000.
Wakati huo huo,
mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Waamuzi wasaidizi ni Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa
Dar es Salaam wakati mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment