Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 14, 2012

CASTLE LAGER YATAMBULISHA SUPERFANS KUTOKA TANZANIA KABLA YA SHINDANO KUBWA LA BARA LA AFRIKA


Washindi wa Castle Lager Super fan Yahaya Hamza toka mkoani Mwanza na Filbert Nestory toka Dar Es Salaam wakiwa na Meneja wa Bia ya Castle lager Kabula Nshimo kwenye kikao na waandishi wa Habari kilichokuwa kikiwatangaza kuwa washindio na kujiandaa kuiwakilisha Nchi kwenye fainali ya mataifa ya Afrika ambapo wataungana na washindi wa nchi nyingine kuunda timu ya ushangiliaji ya Afrika United Team.
Castle lager wadhami wa mchezo wa mpira Afirika wametambulisha Superfans wawili ambao watawakilisha Tanzania katika fainali za kombe la Afica litakalofanyikia Afrika kusini mwanzoni wa 2013.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar Es Salaam Meneja wa castle Lager Kabula Nshimbo aliwataja washindi hao kuwa ni Yahaya Hamza na Filbert Nestory ambao wamejipatia nafasi ya moja kwa moja kwenda nchini Afrika kusini kushiriki katika kuunda timu ya Ushangiliaji itakayojulikana kwa jina la Castle Lager United team
Miezi kadhaa iliyopita superfans wetu walishiliki kwenye ushindani wa kijamii kupitia vyombo vya habari ili kubaini Superfans wanane kutoka nchi nne za Kiafirika,ambazo ni Tanzania,Zimbabwe,Zambia na Swaziland kwa ajili ya safari ya kipekee iliyolipiwa kwenda kuangalia kombe hilo la kiafirika.
Baada ya mzunguko wa kwanza wa shindano hilo kukamilika Tanzania, Superfans hao walipunguzwa na kubakia wachache ambapo watu mbalimbali nchini walichangua Superfans bora waliojitoa kwa ajili ya timu zao na kuvaa vizuri. Uchaguzi huu ulifanyika kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na mwishoni Firbert na Yahaya walitambulishwa kuwa washindi.
“Tunavyojiandaa kwa ajili ya mashindano ya kombe la Afrika 2013 yatakayofanyika Arika kusini tunataka kutengeneza mazingira ya furaha na shangwe kuhusu shindano  hilo,na pia kufanya mashabiki wote wa Afrika kushabikia timu zao na ndio maana tumefanya kampeni ya Superfans hao ambao wanashinda safari na tiketi ya kwenda kwenye fainali za kombe la Afrika,” alisema Bi Mshimo.
 Alisema, “mashabiki wanaendelea kuwa na umuhimu sana kwenye mashindano kama haya ya mpira na nivizuri kuwapongeza na kuwapa nafasi kama hii ya kipekee inayotokea mara moja kwenye maisha ya mtu.”
Washindi wote wawili watapata nafasi ya kumuangalia mcheza mpira wanaye mpenda moja kwa moja kiwanjani nchini Afrika Kusini. Katika washindi hawa wawili, Filbert ni mshabiki mkubwa wa Didier Drogba  wakati mwenzake Yahaya anampenda sana Yaya Toure.
Kwa ajili ya safari yao ya kwenda Afika kusini,Watanzania hao wawili watapumzika siku mbili katika hoteli ya Push iliyopo Johannesburg.p  Pia mashabiki hao, watatalii sehemu kadhaa ya mji wa Johannesburg na mwisho kabisa wata udhuria fainali za kombe la Afika 2013 kama wageni maalum wa Castle lager.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...