Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 3, 2012

JUMUIYA YA WAZAZI KURUDISHA MALI ZAKE ZILIZOVAMIWA KINYUME CHA SHERIA



DAR ES SALAAM, Tanzania

JUMUIYA ya Wazazi nchini imesema itahakikisha inarudisha mali zake zote zilizovamiwa kinyume cha sheria ikiwemo Shule ya Kaole ambayo ni ya kihistoria kati ya nchi ya Msumbiji na Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema huo ni mkakati wa uongozi mpya uliyoingia madarakani hivi karibuni.
Alisema kitendo alichofanya Mkurugenzi wa shule za Green Acle, Julian Bujugo hakikubaliki kwani kimevunja mikatiba ya nchi mbili ya kulifanya eneo hilo kuendelea kuwa la kumbukumbu ya wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji.
“Haitafika Januari mwaka ujao Shule ya Kaole itakuwa imeisharudishwa mikononi mwa Jumuiya kwani shule ile ni ya nchi mbili naitaendelea kuwa ya kumbkumbu ya FLELIMO”alisema Bulembo.
Bulembo alisema eneo la Kaole haliwezi kuuzwa na kumilikiwa na watu wengine na baadala yake litabaki kuwa la watu wa msumbiji kutokana na ukweli kwamba kuna makaburi ya ndugu zaao ambapo hutembelea eneo hilo mara kwa mara.
“Tumemuita Bujugo kesho tukutane naye na kumjulisha kuwa alichofanya ni ukiukaji wa sheria hivyo anapaswa kuanza mchakato wa kukabidhi shule hiyo haraka kwa jumuiya”alisema.
Akifafanua zaidi, Bulembo alisema Jumuiya hiyo ilikumbwa na matatizo mengi hapo awali kutokana na baadhi ya watendaji kutokuwa waaminifu kuuza baadhi ya mali.
Alisema baada ya uongozi mpya kuyabaini hayo, inawatahadharisha wale wote waliyovamia mali za jumuiya hiyo kutambua kuwa wakati umefika kwa kuzirudisha hata kama ni kwa fidia kidogo watakayopewa na Jumuiya kinyume chake watawaburuza mahakamani.
Akizungumzaia maendeleo ya shule za jumuiya hiyo, Bulembo alisema zipo shule 71 ambapo kati hizo, 53 zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma.
Alisema kutokana na hali hiyo wamefikia muafaka na Kamati ya Shule hizo kuanza mchakato wa kuzibadili zile 18 ambazo hazifanyi fizuri  kuwa za ufundi (VETA), ambapo alisema Veta yao itakuwa tofauti kwani itapokea vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na siyo kidato cha nne, kwani kundi hilo linasahaulika pindi liingiapo mitaani.
“Niwatowe wasiwasi wazazi wenzangu kuwa Jumuiya haina mpango wa kuuza baadhi ya shule zake zinazofanya vibaya bali mpango wetu ni kuziimalisha kiufundi ili ziweze kupokea kundi hilo la watoto wetu wanaomaliza elimu ya msingi” alisema Bulembo
Vilevile alisema kuwa hivi sasa shule zao siyo za huduma tena bali zitakuwa za kibiashara kama nyingine kwa sababu sera zilizoanzisha shule hizo awali zimepitwa na wakati.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...