Mabondia Francis Miyeyusho (kulia) akitambiana na Nasib Ramadhan
(kushoto) huku wakishuhudiwa na Mohamed Bawazir mratibu wa pambano hilo
la ubingwa wa mabara wa Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), uzito wa
Bantam, Dar es Salaam leo, Pambano hilo litafanyika Siku ya Uhuru wa
Tanzania Bara Desemba 9, mwaka huu kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es
Salaam. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Ramadhan akitambiana na Miyeyusho (kulia)MABONDIA Francis Miyeyusho na Nasib Radhaman wametambiana kila mmoja kumchakaza mwenzie katika pambano la Ubingwa wa Mabara la uzito wa Bantam litakalofanyika Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara kesho kutwa kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam.
Mabondia hao walitambiana mbele ya waandishi wa habari, ambapo waliwataka wapenzi wa ndondi kwenda kwa wingi kushuhudia jinsi watakavyooneshana umwamba.
Bondia Nasib Ramadhan alisema haoni sababu ya kushindwa kumchakaza 'Babu' Miyeyusho kwa vile amendaliwa vizuri na
kocha wake kwa ajili ya pambano hilo.
"Nashukuru Mungu pamoja na kocha wangu kwa kuniandaa vizuri, namwambia huyu babu kuwa sioni sababu ya
kushindwa kumpiga kwani nimejiandaa vizuri na namjua vilivyo naamini hata mashabiki wake Miyeyusho watanishangilia
mimi siku hiyo baada ya kumpatia kichapo", alitamba Ramadhan.
"Naye Miyeyusho alitamba kuwa hajawahi pigwa bondia yeyote ipokuwa Rashid Matumla, lakini kwa vile mtoto huyu kaniambia mi babu , basi ajiandae jinsi ntakavyombabua, mimi huwa siongei mengi nimekuwa Bubu, matendo yangu ulingoni, njooni mshuhudie", alijinasibu Miyeyusho.
Mratibu wa pambano hilo, ambaaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya DarWorld Links LTD, Mohamed Bawazir aliseama kuwa maandalizi ya pambano hilo laa kukata na shoka kwa asilimia kubwa yako tayari na kwa mba kesho mabondia watapimwa uzito kwenye Uwanja wa Karume.
Bawaziri alisema kuwa pambano hilo ambalo mgeni wake rasmi atakuwa Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara, litaanza saa 9 alasiri, ambapo pia wapenzi wa soka watawekewa screen kwa ajili ya kuangalia
mechi za kimataifa wakiwa ukumbi huo wa PTA.\
Aliwataja viongozi wengine watakaoshuhudia pambano hilo kuwa ni, Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Mathayo David, Meya wa Kinondoni, Mwenda na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Alitaja mapambano ya utangulizi kuwa ni;Juma Fundi vs Fadhil Majia, Mohamed Matumla vs Doi Miyeyusho, Ibrahim Class vs Said Mundi, Fred Sayuni vs Deo Samwel na Hassan Kidebe vs Baina Mazola
.Super D atasambaza DVD zake Mpya katika mpambano wa Franisic Miyayusho VS Nassibu Ramadhan litakalofanyika katika ukumbi wa PTA SABASABA atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
NASSIBU KUSHOTO NA MIYAYUSHO |
No comments:
Post a Comment