Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe
mwenye suti akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo
Aman Kisamfu kabla kuzindua safari ya treni ya abiria kwenda Mwanza leo mchana
katika Stesheni ya Dar es Salaam.
WAZIRI wa Uchukuzi leo mchana amezindua
rasmi usafiri wa treni za abiria toka Dar es Salaam hadi Mwanza,
hivyo kutimiza ahadi ya Serikali iliyotolewa Bungeni kipindi cha
Bajeti mwaka huu kuhusu
kurejesha huduma hiyo.
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa amefuatana na viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu
wa Wizara, Injinia Omar Chambo na Mtendaji Mkuu wa TRL, Injinia Kipallo
kisamfu aliruhusu treni hiyo kuondoka stesheni ya Dar es Salaam Saa
8:30 mchana huku abiria wakishangilia na kudai huduma hiyo
iendelezwe zaidi na zaidi.
Usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar
na Mwanza ulisitishwa Desemba 2009 kufuatia maamuzi ya iliyokuwa
menejimenti ya Kampuni ya RITES kutoka India .
Treni hiyo ikiwa imefunga Mabehewa 16
yenye abiria wapatao elfu moja inatarajiwa kuingia Mwanza Jumapili
asubuhi na kupokewa na Mhe. Naibu Waziri wa UCHUKUZI, Dkt. Charles Tizeba
na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza.
Akiongea na viongozi na Wafanyakazi
baada ya ufunguzi huo, Dkt. Mwakyembe aliwapongeza Wafanyakazi wa
TRL hasa mafundi wa karakana za Dsm na Morogoro kwa kazi kubwa ya
kufufua Injini na Mabehewa hivyo kulikolea Taifa mabilioni ya pesa ambazo
zingetumika kukodisha vifaa hivyo kutoka Afrika ya Kusini, India ama
nchi nyingine.
Treni ya abiria ya Mwanza itakuwepo kwa
kuanzia mara mbili kwa wiki Jumanne na Ijumaa kama ilivyo kwa treni
ya Kigoma na baadaye kuongezeka jinsi injini na mabehewa
yatakavyokuwa yanaongezeka kutengenezwa.
|
No comments:
Post a Comment