CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinaendelea na
maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel, Bagamoyo mkoani Pwani.
Kama
tulivyosema wiki iliyopita kuwa mkutano huo unatarajiwa kushirikisha
wanachama zaidi ya 100, ambao kushiriki kwao itabidi wathibitishe kwa
njia ya maandishi kwa maana ya email ili uwepo wao uweze kuthaminika.
Lakini bado
kuna mwitikio mdogo wa wanachama wanaothibitisha ushiriki wao, ambapo
hadi kufikia leo saa tano asubuhi waliothibitisha ni 22 tu, hivyo
tunasisitiza wengine wafanye hivyo haraka na tusikubali kufanya mambo
kwa mazoea na mwisho wa kuthibitisha ni Jumamosi Desemba 15, saa kumi
alasiri na watakaokwama kufanya hivyo watahesabika wamekosa sifa ya
kushiriki mkutano.
Tunaomba
wanachama wote ambao wanatarajia kuhudhuria mkutano huo wathibitishe
ushiriki wao kwa Katibu Mkuu wa TASWA kwa njia ya email:mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com.
Kamati ya
Utendaji ya TASWA inaendelea na juhudi za kutafuta wadhamini kwa ajili
ya Mkutano Mkuu, ambapo kiasi cha Sh. Milioni 20 kinahitajika
kufanikisha mkutano ikiwa ni gharama mbalimbali ikiwemo chakula, malazi,
usafiri kwa wanachama wa Dar es Salaam, pamoja na usafiri na malazi kwa
wanachama wanaotoka nje ya Dar es Salaam.
Tayari wadau
watatu wamejitokeza kupiga jeki mkutano huo, ambapo Alhamisi Desemba 13
saa tano asubuhi mgahawa wa City Sports Lounge Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto atatangaza mdhamini mmoja ambaye tutakuwa tumemalizana naye.
Kiasi cha
fedha kinachohitajika ni kikubwa sana, hivyo bado jitihada zinaendelea
kutafuta wadhamini wengine kuhakikisha mkutano unakuwa wa mafanikio
makubwa na tunaomba wenye nia ya kushirikiana nasi wafanye hivyo.
Licha ya
wanachama pia tunatarajia katika mkutano huo pia watakuwepo wadau
mbalimbali wa TASWA wakiwemo waandishi wakongwe wa habari za michezo
ambao watapewa nafasi ya kuzungumza.
Wanachama wa
TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama,
Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu
waandishi wa habari za michezo kwa ujumla.
Pia kutakuwa
na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo ili wawe
na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo
itajadiliwa kwenye mkutano huo.
Kamati
ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze
kujitegemea kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini
imeamua kwanza iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya
jambo hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe
kama ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye Mkutano Mkuu.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
No comments:
Post a Comment