Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi akiwa Mwenyekiti wa wake za viongozi,
Germina Lukuvi mara baada ya timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens)
iliporejea nchini na Kombe la Michiuano ya Kimataifa iliyofanyika nchini
Singapore.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa
Queens’ wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam leo wakitokea Singapore walikokuwa wakishiriki michuano ya
Kimataifa na kutwaa
Kombe la michuano hiyo.
Mlezi wa Chaneta kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Ain Sharif
akikabidhi kitita cha sh. 500,000 ikiwa ni kama zawadi kwa timu hiyo
baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa yaliyofanyika
Singapore na Taifa Queens kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Wachezaji
na viongozi wa timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Quees) wakiwa katika
picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili leo kwenye uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Singapore.
Na Mwandishi Wetu
TIMU
ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’ imerejea kwa kishindo
leo baada ya kushiriki na kutwaa Kombe la michuano ya Kimataifa
iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani Asia.
Taifa Queens ilitwaaa ubingwa huo baada ya kuingia fainali
ikiwa na pointi 10 ikicheza na timu ya Malasia iliyokuwa na pointi 4 ambapo
ilifanikiwa kuifunga magoli 45-38.
Akizungumza baada ya kurejea, Mwenyekiti wa Chama cha
Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alisema maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini
kocha aliwapa wachezaji mbinu za kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.
“Hii imetusaidia sana maana kocha mwenyewe ni kijana hivyo
anambinu za kisasa kitu kilichotusaidia wakati tukiwa ugenini, hakuna kitu
kizuri kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa ugenini huku wazungu ambao ni wenyeji
wa mashindano hayo wakiwa penbeni,” alisema Bayi.
Kwa upande wake Kocha wa Taifa Queens, Mary Waya alisema
mashindano yalikuwa ni magumu anawapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambao
umemuweka pazuri yeye pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.
“Kila kitu unatakiwa umtangulize mungu, akili, na nguvu
ndio zinafuata naimani wachezaji wangu walikuwa makini na kujua nini wamekifuata
huko, akili ni kitu cha muhimu ukiwa mchezoni hivyo mimi sina la kusema zaidi
ni kumshukuru mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Kocha huyo ambaye ni
Mmalawi.
Kocha huyo alisema amefurahishwa na ushindi huo na kwamba kwasasa
anajipanga kuifua timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia.
Naye Nahodha wa timu hiyo, Lilian Sadolin alisema
anamshukuru mungu kwa ubingwa huo pia Watanzania wanatakiwa kuendelea kuwapa
sapoti katika mashindano mbalimbali.
No comments:
Post a Comment