Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa akitoa neno fupi la kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kabla haja kabidhi madawati hayo. |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Sadiki akiteta jambo na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa Juma Fundi |
Walimu na wanafunzi wakiwa katika makabidhiano hayo. |
wanafunzi wa shule hizo wakiwa katika hafla hiyo ya makabidhiano. |
Na Mwandishi Wetu
SHULE za Sekondari za Majani ya Chai na Ilala zilizopo Manispaa ya Ilala Dar es Salaam zimepata msaada wa madawati kutoka Kampuni ya TSN Group ili kukabiliana na adha ya wanafunzi kukaa chini.
Vifaa vilivyokabidhiwa na kampuni hiyo ni viti 180 na madawati 90, ambavyo vitapunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati wakiwa darasani.
Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Farouk Baghozah akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo, alisema kuwa kampuni hiyo imeshasaidia shule takriban 8.
"Tumekuwa tukisaidia madawati na sasa ni miezi minne tangu tuanze mchakato huu hapa nchini kwa kushirikiana na kampuni yetu iliyoko Uingereza," alisema Baghozah.
Akikabishi msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki aliipongeza Kampuni ya TSN pamoja na Diwani wa kata hiyo, Bonah Kaluwa kwa kusaidia sekta ya elimu.
Aliwataka wazazi kujitolea katika shughuli za maendeleo badala ya kuiachia Serikali kununua madawati na kujenga majengo ya shule.
Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa mkoa aliwata watu wote waliovamia maeneo ya shule kuondoka mara moja na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wake kuahakikisha anakutana na wavamizi hao kuzungumzia suala hilo.
"Wale wote waliopo maeneo ya shule, wakiwemo wamiliki wa msikiti uliopo ndani ya Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, tunawaomba waondoke ili kupisha uendelezaji wa shule katika eneo hilo," alisema Sadiki.
Diwani wa kata hiyo, Bonah Kaluwa alisema utoaji wa madawati hayo ni muendelezo wa kampeni yake ya kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika shule mbalimbali zilizopo katika kata yake, ambapo tayari shule zote tano zimenufaika na mpango huo kwa kupata madawati 500 huku kila moja ikipata madawati 100.
Msaidizi wa Mratibu Elimu wa Kata ya Kipawa, Aina Mlewa alisema licha ya kupata msaada huo, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa na pamoja vyoo ambapo wanafunzi huchangia choo kimoja na walimu.
No comments:
Post a Comment