Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck (kulia) akizungumza na Naibu waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene nje ya ukumbi wa bunge wakati alipofika bungeni hivi karibuni, kwa ajili ya utambulisho wa mbio za Uhuru Marathon.
*******************************
Mwandishi Wetu
MASHINDANO
yambio ndefu ambayo yatajulikana kama Uhuru Marathon, yanatarajiwa
kuzinduliwa rasmi leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenella Mukangara katika hoteli ya JB Belmonte iliyopo Mtaa wa
Azikiwe, Dar es Salaam.
Uhuru Marathon inazinduliwa huku tayari mashindano hayo yakiwa yametambulishwa rasmi kwa wabunge katika bunge lililopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Uhuru
Marathon, Innocent Melleck alisema, katika uzinduzi huo utakaofanyika
kuanzia saa 12 jioni, viongozi wa kada mbalimbali watahudhuria.
“Kila
kitu kwa ajili ya uzinduzi huo kimekamilika na watakuwepo viongozi wa
kada mbalimbali wakiongozwa na Dk. Fenella, tunataka kufanya kitu
kikubwa zaidi kwa nchi hii,” alisema.
Mratibu
huyo alisema, lengo la mbio hizo ni kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa
kukumbuka, kuzingatia na kuuenzi urithi waliaochiwa na viongozi
waliopigania uhuru wa nchi hii.
Alisema,
urithi huo ambao utakuwa ukikumbukwa kila mwaka kupitia mbio hizo ni
upendo, mshikamano, umoja na amani iliyopo. Melleck anasema mbio hizo
zitakuwa zikifanyika kila mwaka na zitaanza rasmi hapo mwakani.
Katika
mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia
mbio za kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na
Full Marathon yenyewe itakayokuwa kilomita 42.
Mratibu
huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi
wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia
zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
“Hapa
tunachotaka kufanya katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile
viongozi maarufu wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wetu serikali ili
kushiriki, kwa kudumisha amani na upendo.
“Pia
tutahakikisha kama mbio za kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia
watu wenye mahitaji mbalimbali na tayari tuna uhakika mkubwa wa
wanariadha maarufu zaidi duniani kushiriki,” anasema.
Mratibu
huyo anafafanua kuwa wamejipanga mno katika hilo ili kuhakikisha
wanafanya mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.
Waandaaji
wa mbio hizo ambao ni Kampuni ya Intellectuals Communication Ltd kwa
ushirikiano na waandaji wa mbio za Berlin Marathon zilizo maarufu zaidi
duniani.
No comments:
Post a Comment