Uongozi wa Jumuiya ya watanzania waishio Marekani, unawashukuru kwa dhati wote walioshiriki kuandaa sherehe
ya kumkaribisha Balozi Manongi na Naibu wake Balozi Mwinyi.
Tunayo furaha kubwa
kwenu kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha sherehe hii.
Msaada
wenu wa kifedha na vyakula mbali mbali viliwezesha kufanikiwa kwa
maandalizi hadi kufanyikwa kwa sherehe yetu na kufurahiwa na kila
aliyehudhuria.
Pia tunawashukuru kwa Amani na Utulivu tulioonyesha. Wageni wetu waalikwa Balozi Manongi na Naibu Mwakilisha Balozi Ramadhani
Mwinyi pamoja na familia zao walifurahi sana.
Balozi manongi ameomba tuwafikishie salam zake binafsi za shukurani kubwa.
Tunaomba mzipokee.
Kwa mara nyingine tunawashukuru nyote kwa ushirikiano mkubwa. Pia tunaomba
tuendelee na ushirikiano na mshikamano kati yetu. M/Mungu azidi kuibariki
Tanzania. amina
Ahsanteni Uongozi: New York Tanzanian Community
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment