Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa Tamko la Mount Meru la kuwalinda waandishi wa
habari wakiwa kazini Afrika Mashariki, Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika Bw. Francis Stolla akizungumza machache wakati wa uzinduzi
huo ambapo alisisitiza umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika
kujenga Demokrasia na Utawala Bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki na
kati. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed
Tibanyendera (wa tatu kushoto), Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa (kulia),
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania
(UTPC) Bw. Abubakar Karsan ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa MISA-TAN
Bw. Tumaini Mwailenge (kushoto).
Mtangazaji
wa Radio Clouds Fm Regina Mwalekwa akisoma Tamko rasmi la Mount Meru
lililoandaliwa siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani
yaliyofanyika Mei 3-4 mwaka huu jijini Arusha yaliyohudhuriwa na
washiriki mbalimbali toka vyombo vya habari, redio za jamii, jumuiya
mbalimbali za Kimataifa, Taasisi za mafunzo ya tasnia ya habari na
mifuko ya Maendeleo ya Tasnia ya habari kutoka Tanzania, Kenya, Uganda
na Rwanda.
Mgeni
rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla (wa
pili kulia) akizundua rasmi Tamko la Mount Meru linalozunngumzia
vipengele mbalimbali vitakavyowalinda waandishi wa habari Afrika
Mashariki.
Mgeni
rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla
akionyesha Tamko rasmi la Mount Meru la kutetea Uhuru wa Vyombo vya
Habari kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla
akizindua rasmi CD ya wimbo ulioimbwa na Mjomba Band unaoitwa "Uhuru
Wangu" uliopigwa kwa mara ya kwanza wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika katika Hoteli ya Naura
Springs jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa
Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera ( wa pili kushoto), Mjumbe wa MCT
Bw. Allan Lawa (kulia) na Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa
habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan (kushoto).
Sasa umezinduliwa rasmi....Kaa tayari kuusikiliza katika radio mbalimbali na mitandao ya kijamii hapa nchini.
Mjumbe
wa MCT Bw. Allan Lawa akizungumza umuhimu wa waandishi wa habari
kujali maslahi mapana ya taaluma ya uandishi wa habari katika mchakato
wa kuandika Katiba mpya kupitia mabaraza ya Katiba ya Wilaya.Vile vile
alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika
kujadili rasimu ya Katiba mpya iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa
Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal ili kuhakikisha Taifa linapata Katiba
Mpya inayojali Uhuru wa vyombo vya Habari hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania
(UTPC) Bw. Abubakar Karsan akifafanua jinsi Mfuko wa Mwangosi
utakavyokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa
kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa
amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo
hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi
Mwangosi na mshindi atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na
waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane
Mihanji akiteta jambo na Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) (Wa pili kushoto) na Bi. Rose Mwalimu kutoka
UNESCO (wa pili kulia).
Mdau
kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) akitoa
maoni yake juu ya tamko la Mount Meru kwenye uzinduzi uliofanyika leo
jijini Dar katika Hoteli ya Peacock.
Baadhi
ya waandishi wa habari waandamizi nchini kutoka kushoto ni Shermax
Ngehemera Mhariri wa The African, Hamis Mzee wa MCT na Mhariri wa zamani
wa Mwanaspoti ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah.
Wadau mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari waliohudhuria uzinduzi wa tamko la Mount Meru.
--
Kufuatia Mkutano wa Wadau wa Habari Afrika Mashariki waliadhimia yafuatayo;-
1.Serikali zote nchi za Afrika Mashariki zihakikishe kuwa Katiba za nchi zao zinakuwa na vipengele kwa ajili ya:
-Kuwa na tasnia ya habari ambayo ipo huru, salama na yenye kujitegemea ikijumuisha usalama wa wanahabari.
-Sheria nyingine zote ziheshimu Katiba za nchi zikiendana na vyombo na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.
2. Wamiliki wa vyombo vya habari wafanye marekebisho ya miundo ambayo itazingatia yafuatayo;
- Uendeshaji bira- Ikiwa ni pamoja na masuala ya Ajira, Mishahara, Mikataba, Motisha na Marupurupu mengine ya kifedha.
- Viendeshwe kwa kufuata na kuheshimu miiko ya Kitaaluma.
-Kuhakikisha kuwa wanahabari wote wanakuwa na Bima.
-Vyumba
vya habari viongeze uwekezaji katika mitandao ya kijamii pamoja na
utoajji elimu kwa wanahabari kuhusu mitandao binafsi yaani Blogs.
3.
Baraza la Habari lishirikiane na taasisi na vyama vya kitaaluma vya
wanahabari ili kudumisha na kulinda ueledi na umoja katika tasnia ya
habari.
4. Wanahabari waanzishe vyama vya wafanyakazi ili kuwezesha na kuongeza mapatano na makubaliano ya hiari sehemu za kazi.
5. Wamiliki wa vyombo vya habari walinde na kutetea usalama wa wanahabari na vyombo vyao kupitia
-Wamiliki wa vyombo vya habari kuweka na kuzingatia taratibu za usalama sehemu za kazi
-Wamiliki
wa vyombo vya habari wahakikishe wanwapatia waandishi wa habari vifaa
vya usalama au vya kujikingia na hatari na wawezeshe mafunzo juu ya
taratibu za usalama.
-Kujumuisha mitaala ya mafunzo ya usalama na ulinzi katika taasisi zote za mafunzo ya uandishi wa habari.
- Wanahabari wao binafsi wachukue vipaumbele na tahadhari katika usalama wao binafsi.
6.
Jumuiya ya Afrika Mashariki lizitake nchi wanachama wake ambao walitia
sahihi itifaki ya Udhibiti wa Tovuti wajiondoe katika Mkataba huo ikiwa
ni njia moja wapo ya kudumisha utawala bora na uwajibikaji.
7.
Serikali za Afrika Mashariki zifanya juhudi katika kuwezesha
uanzishwaji wa mfumo wa kisheria wa kuruhusu uendeshaji bora wa mitandao
ya kijamii na wakati huo huo wakilinda uhuru wa wadhibiti ili kuboresha
na kuendeleza uhuru wa mitandao ya kijamii katika eneo la Afrika
Mashariki.
No comments:
Post a Comment