TAMASHA la Mastaa
Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha wasanii
Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya Rais wa Marekani, Baraka Obama.
Mwenyekiti
wa
Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim Taalib alisema jana kuwa
wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo watakuwa katika
maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti baada ya
sikukuu ya Idd el Fitri.
Taalib
alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga, viongozi mbalimbali na
wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa kuonesha vipaji
vyao katika tamasha hilo.
‘Tumeamua kutoa
nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili washiriki kikamilifu kudumisha
amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na Rais Obama na wasanii
washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika vyombo vya dola mara
tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib.
Mwenyekiti huyo
alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Adam
Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaam nao wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo.
Alisema
sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi nyumba kwa mchezaji
wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na
wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
Wengine
watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola
‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi
wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora
Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mpaka
sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la
hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili
kujikwamua kimaisha.
No comments:
Post a Comment