Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 24, 2013

Soma Taarifa Maalum Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Juu ya Kufungwa Kwa Sehemu ya Barabara ya Kontena,Kanisani-Msikitini hadi Changanyikeni


UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
OFFICE OF THE DEPUTY VICE-CHANCELLOR
(ADMINISTRATION)
P.O. BOX 35091 - DAR ES SALAAM - TANZANIA 
.
Tel.:    022 2410500 - 8 Ext.
2003
 
           022 2410394 - Direct Line
Fax:    022 2410718
Ref:     z1/18
Telegram:  University of Dar es Salaam
E-mail:    dvc-pfa@admin.udsm.ac.tz
Website:   www.udsm.ac.tz 
21  Juni, 2013  
Wanajumuiya Wote

YAH: KUFUNGWA KWA SEHEMU YA BARABARA YA KONTENA—KANISANI/MSIKITINI— CHANGANYIKENI  

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unautaarifu umma kuwa kipande cha barabara kuanzia kumbi za mihadhara ya Yombo 1&2 na Bweni Na. 6 hadi barabara ya Changanyikeni kitafungwa kuanzia Jumapili tarehe 23 Juni 2013.

Barabara inayoanzia kituo cha daladala cha Kontena hadi Bweni Na. 6 ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya Chuo tu, ingawa kwa siku za karibuni matumizi ya barabara hiyo yameongezeka kiasi cha kuhatarisha usalama wa wanafunzi na wafanyakazi wanaotumia kumbi za mihadhara na ofisi zilizopo maeneo hayo.

Kwa hiyo, watu wote waliozoea kutumia barabara hiyo kuelekea Changanyikeni kwa vyombo vya usafiri vya moto, wanashauriwa kutumia barabara ya kawaida inayoanzia au kutokea karibu na tawi la NBC.

Tunawapa pole kwa usumbufu utakaojitokeza kwa kufungwa kwa barabara hiyo.

Prof. Y. D. Mgaya
NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO - UTAWALA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...