Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 20, 2013

Mbowe, Lema wajisalimisha Polisi


Mwenyekiti wa CHADEMA  Fremaan Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema leo wamejisalimisha Polisi  baada ya jeshi hilo kutangaza linawasaka baada ya vurugu ziliztokea jana mjini Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari,  Fremaan Mbowe alisema kuwa wao wamejisalimisha kama polisi walivyosema wanawatafuta na walipofika waliandika maelezo ambapo alisema kuwa polisi waliwaita kwa mambo mawili, moja likiwa ni kwa kuwahoji kwanini walifanya mkutano usio wa halali ambapo alisema kuwa;
"Jambo la kufanya mkutano pasipo kuwa halali sio kweli kwani polisi walituruhusu tukafanye mkutano katika sehemu hile lakini kinachotushangaza tumefanya wamekuja kutupiga mabomu na kusema sio wa halali na kuhusiana na ushahidi msimamo wangu upo pale pale tunao ushahidi wa kutosha na tunamjua aliyerusha bomu Jumamosi, lakini hatutautaoa hadi  Rais atakapounda Tume Huru ya majaji ili wafuatilie suala hili. Hao ndiyo tutawaonyesha ushahidi huo, lakini siyo Polisi hatuwezi kuwapa," alisema Mbowe.
Afande Chagonja akiongea na waandishi wa habari
Kwa upande wa Polisi kupitia Kamishna wa Mafunzo na Operesheni za Kijeshi,  Paul Chagonja akiongea na wanahabari alisema waliwahoji wabunge hao na kuwaomba ushahidi waliokuwa nao kama wanavyodai, lakini waheshimiwa hao hawakutoa ushirikiano.
"Mbowe alisema kuwa ana ushahidi na hata katika vyombo vya habari ametangaza lakini nashangaa tulivyomuuliza hapa amesema kuwa hana ushahidi wowote na wala hajawahi kutamka hivyo sasa sisi kwa kuwa kasema hivyo nitakaa na makachero wangu na tutaangalia jinsi ya kufanya"alisema Chagonja
Aidha alisema kuwa alimuliza mbunge wa Arusha mjini kwanini awali alikuja kuwasifia Polisi baadae akawageuka ilihali alishasema katu hawezi kusema uongo na kuwajibu kuwa, yeye anafuata mwenyekiti wake anachosema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...