Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 14, 2013

warembo wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013


Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.

Ambapo mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu aliyonayo. Pia atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya shilingi 300,000 pamoja na fedha taslimu shilingi 500,000.

Mshindi wa pili;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 300,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 200,000.

Mshindi wa tatu;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 100,000.
Mshindi wa 4 na tano; watapata uthamini wa masomo ya kompyuta ya miezi sita. Mshindi wa nne atapata pia pesa taslimu laki mbili  na nusu na wa 5 laki moja na nusu.Washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha shilingi laki mbili kwa kila mmoja.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
 Muonekano wa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013
 Kila mmoja akiwa na furaha na bashasha.
 Baada ya mkutano na waandishi wa habari warembo walipata nafasi ya kutembelea ofisi za wadhamini wao ambao ni Oriflame Natural Beauty Products zilizopo jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam, na hapo waliweza kupata semina ya kuelezewa jinsi vipodozi vyao vinavyofanya kazi kama pichani unavyoona mwezeshaji akitoa somo kwa warembo.
 Mmoja ya warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 akiuliza swali kwa mwezeshaji.
Kila mrembo akijaribu kuweka kumbu kumbu kwa yale waliyokuwa wakifundishwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...