Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 21, 2013

CHEKIBUDI ASHUKURU MAPOKEZI YA 'DIKTETA'




Na Elizabeth John

MUIGIZAJI wa filamu nchini, Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’ amewashukuru wadau na wapenzi wa kazi zake baada ya kumpokea vizuri na kazi yake inayokwenda kwa jina la ‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri sokoni.
Filamu hiyo inayoonesha ukandamizaji wa familia, imekamilika na kuingizwa sokoni hivi karibuni, ambapo tayari imeanza kufanya vizuri katika  mauzo baadhi ya maeneo ya jijini  Dar es Salaam, ikisambazwa na kampuni ya steps Entertaiment.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chekibudi alisema, filamu hiyo ameiandaa ili kuonesha ukandamizaji uliopo baadhi ya familia katika maisha ya kila siku, na amefarijika kuona iko katika wakati mzuri sokoni.
Alisema baada ya kuangalia hilo, aliamua kuweka wazo lake katika filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi zaidi na ikawa kama ni moja ya kazi za wasanii kuelimisha na kufundisha jamii.
“Unajua unapokuwa msanii unatakiwa kuwa mbunifu katika mambo mengi na ndiyo maana kila kukicha tunaangalia ni jinsi gani tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo yanaepukika,” alisema Chekibudi.
Chekibudi alishawahi kufanya vizuri alipokuwa katika kundi la sanaa la ‘Splendid’, na katika filamu hiyo ya ‘Dikteta’ amewashirikisha nyota wengine kama, Cojack, Philipo, Munira Sultan, Snura Mush, Coletha Reymond pamoja na nyota wengine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...