Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 18, 2013

REDDS MISS KINONDONI TALENT 2013 KUFANYIKA ALHAMIS 21 JUNI UKUMBI WA SHEKINAH GARDEN JIJINI DAR


Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), kwa sasa warembo hao wameshaingia katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam kujinoa kwa ajili ya Redd's Miss Kinondoni Talent 2013 zinazofanyikia ukumbi wa Shekinah Garden Mbezi Beach na Fainali zinafanyika Juni 21 ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip.
---
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
SHINDANO la Redd’S Miss Kinondoni Talent 2013 linatarajiwa kufanyika alhamisi ya Juni 25 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambalo litashirikisha warembo wapatao kumi na mbili ambao watachuana kumpata mrembo mwenye kipaji.
Akizungumza mratibu wa shindano hilo, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.
“Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao “Alisema Ssebo.
Warembo warembo wanaotarajiwa kumenyana ni kutoka katika vitongoji vya Sinza, Ubungo na Dar Indian Ocean ambao kwa pamoja wanaunda Redd's Miss Kinondoni 2013.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...