Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 18, 2013

Polisi wafafanua sababu ya kulipua mabomu ya machozi leo Arusha



Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.

Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa  mabumu yalianza kusikika.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee...

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...