JUMLA
ya timu nane zimethibitisha kushriki katika bonaza la soka klabu ya
Break Point lililopangwa kufanyika Jumapili Juni 23 kwenye viwanja vya
Survey (Chuo Kikuu cha Ardhi).
Mkurugenzi wa Breake Point Outdoor Distributors, Daudi Machumu
alizitaja timu ambazo ambazo zitashiriki katika bonanza hilo
lililodhaminiwa na kampuni ya bia ya Seregeti (SBL) kuwa ni, Rose
Garden, Survey, Mbezi Beach na Boko Veterans.
Machumu
alisema kuwa timu nyingine ni Clouds Media Group, Magogoni, Umoja na
waaandaaji, Break Point ambayo itakuwa chini ya Rodrick “Neymar”
Mwambene. Alisema kuwa bonanza hilo limepangwa kuanza saa 2.30 asubuhi na madhumuni yake ni kuwakutanisha wadau wa michezo na kubadilishana mawazo.
“Lengo
kubwa ni kupromoti michezo na kujadili mambo mbali mbali, kampuni ya
Break Point Outdoor Distributors ni wadau wakubwa wa michezo na sanaa,
tumedhamini mashindano ya urembo na shughuli nyingine, bonanza hili ni
fursa pekee kwa wadau kukutana na kustarehe kwa pamoja huku wakipata
vinywaji ambavyo vitauzwa kwa bei ya promotion na nyama choma,” alisema
Machumu.
Alisema
kuwa pia kutakuwa na bia za bure kwa timu shiriki na kuwataka
kuzingatia muda kwani wachezaji wa Ligi Kuu na Ligi nyingine
hawaruhusiwi na usimamizi utakuwa mkali. “Hii ni fursa kwa wachezaji
walioachana na mpira wa miguu wa ushindani, tunataka timu kuzingatia
hayo,” alisema.
Machumu
alisema kuwa wameandaa burudani mbali mbali ili kunogesha siku hiyo
muhimu sana kwa wadau wa michezo. “ Natoa wito kwa mashabiki kufika na
timu kuzingatia muda, kwani mtindo utakaotumika utakuwa wa ligi,”
alisema.
No comments:
Post a Comment