Beki wa timu ya Faru Boys Nassoro Dibagula (kushoto) akitoa mpira
katika eneo la hatari mbele ya Abdalah Juma wa Mapambano katika mechi
ya ufunguzi wa michuanoa ya vijana wenye umri chini ya miaka17 ya
Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke, uliofanyika kwenye uwanja wa
Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013. Faru Boys ilishinda 1-0.
Beki wa mapambano Hamisi Hassan akimvuta jezi beki wa Faru Boys
Nassoro Dibagula katika mechi ya ufunguzi wa michuanoa ya vijana wenye
umri chini ya miaka17 ya Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke,
uliofanyika kwenye uwanja wa Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013.
Faru Boys ilishinda 1-0.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki, akikagua timu
wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa
kisoka wa Temeke ambapo Faru Boys football ilichuana na timu ya
Mapambano katika mechi ya ufunguzi
Timu
ya Mbaspo Academy ilifanya mauaji juzi Jumanne kwa kubamiza bila huruma
timu ya Mbeya Sekondari 6-0 katika mashindano yanayoendelea ya vijana
chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa. Mechi
hiyo ilichezwa kwenye kiwanja cha Magereza mkoani Mbeya.
Washindi
walifungua kitabu chao cha magoli katika dakika ya sita kupitia kwa
mshambuliaji wao mahili Jackson Mwaibale aliyefunga magoli manne peke
yake. Mshambuliaji huyo kinda aliifungikia tena timu yake magoli matatu
katika dakika za 16, 20 na 74. Wanafunzi wa shule ya
sekondari Mbeya waliokuja kushangilia timu yao walijikuta kwenye hali ya
kukata tamaa baada ya timu yao kuwanyong’onyesha na wapinzani wao
Mbaspo.
Peter
Noah, mshambuliaji mwingine hatari wa timu ya Mbaspo, aliifungia tena
timu yake katika dakika ya 30. Alikua ni yeye tena katika dakika ya 68
alipoitimisha kalamu ya magoli baada ya kuwapita walinzi wa Mbeya
Sekondari na kumuacha golikipa akiduwaa baada mpira kutinga wavuni.
Kwa
upande mwingine timu ya Faru Boys football walipata ushindi mwembamba
wa 1-0 dhidi ya wapinzania wao Mapambano katika mechi ya ufunguzi ya
ARS, katika mkoa wa Temeke uliofanyika katika uwanja wa Twalipo jumanne
jioni jijini Dar es Salaam.
Timu
zote zilianza mchezo kwa kasi na babada ya kosa kosa za hapa na pale
hatimaye Yohana Joseph ilifanikiwa kuitoa kimasomaso timu yake
alipounganisha krosi kutoka upande wa kushoto ambayo iliingia moja kwa
moja wavuni. Goli hili lilipokelewa kwa furaha na washabiki wa Faru.
Mchezo
mwingine wa Another Airtel Rising Stars, mkoa wa Ilala, ilichezwa
kwenye kiwanja cha soka cha shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa
ambapo timu ya Amana Shooting ilishinda 2-0 dhidi ya Msimamo Youth
Academy. Magoli hayo yalipatikana kupitia kwa Isiaka Mohamed dakika ya
22 na Ally Shaban dakika ya 68.
Mkoa
wa Mwanza ulitarajia kuzindua mechi zake za ARS ngazi ya mkoa leo, Juni
26 wakati Morogoro na Mbeya walitarajiwa kuendeleza na mechi za
mashindano hayo leo, Juni 26, 2013.
Wakati
huo huo, mkoa wa kisoka wa Kinondoni umetangaza kombaini yao ya
wachezaji 15 watakaowakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya Airtel
Rising Stars ngazi ya Taifa yatakayofanyika wenye uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 7.
Wachezaji
hao ni Hamza Mohamed, Hamza Abdallah, Twalib Athuman, Fred Bakari,
Hazzad Jumanne, Salim James, Abubakary Mohamed, Willy Kalolo, Didas
Proches, Mustafa Yusuf, Rashid Khalifan, James Msuva, Isiaka Lukana,
Ally Amin na Shabani Idd.
No comments:
Post a Comment