Na Elizabeth
John
WAKATI zoezi
la kuchukua na kurudisha fomu za kugombea uongozi wa Chama Cha Tenisi Tanzania
(TTA), lilifika tamati tarehe Juni 17, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Denis Makoi
amechukua fomu ya kutetea kiti hicho.
Wagombea 14
wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho na
ucahaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Juni 22 jijini Dar es Salaaam.
Kwa mujibu wa Ofisa
Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, wagombea wengine
waliochukua fomu ni Mtangazaji wa Magic FM, Fina Mango na Mathisut Sele Mbajo
ambao pia wanawania Uwenyekiti wa chama hicho.
Alisema
wagombea wengine waliojitokeza kuchukua fomu ni Joyce Marwa akiitaka nafasi ya
Uhasibu, William Kallaghe aliyejitosa ukatibu mkuu, Josima Mutale anawania
ukatibu msaidizi huku wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kiango
Kipingu, Swalehe Malimbo, Gilbert Peter, Majaliwa Majuto, Nico Jonas, Morris
Loje na Ismail Ngulingo.
“Zoezi hili
limeenda salama, mimi nawasisitiza tu wadau mchezo huu wawachague viongozi
ambao wanaamini watawapa ishirikiano wa kutosha katika kipindi chake cha
uongozi, siku ya usaili kwa wagombea hao itatangazwa mapema kabla ya siku ya
uchaguzi,” alisema Chacha.
No comments:
Post a Comment