Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 9, 2013

Aisha Bui akana kukamatwa na 'unga' Brazili, adai yu salama Afrika KusiniMWANADADA anayetamba kwenye filamu nchini, Aisha Bui amekanusha taarifa kwamba amekamatwa na dawa za kulevya na kufungwa kifungo cha miaka mitano nchini Brazil.

Akizungumza na MICHARAZO kutoka Afrika Kusini, Aisha Bui alisema ameshtushwa na taarifa hizo za kunaswa na 'bwimbwi' Brazili, ilihali yeye yupo Afrika Kusini salama wa salimini.
Aisha alisema angependa kuwafahamisha watanzania kwamba yu salama na wazichukulie taarifa hizo kama uzushi kwa sababu hajawahi na wala hajishughulishi na biashara hiyo ya 'unga'.
Pia mwanadada huyo alitupia ujumbe katika 'wall' yake Facebook akisisitiza suala hilo kwa kuandika;
Dear Friends, Fans n Family Naskia kuna habari flani mbaya zimetolewa na baadhi ya vyombo vya habari, napenda kuwajulisha wote kua hiyo si kweli Mimi ndio kweli niko safari lkn niko salama salmin Hakuna kitu Kama Hicho n namuomba mungu aniepushe na mambo hayo. Niko poa Kabisa n nawapenda wote.

Alipoulizwa kama kuna hatua zozote atakazochukua kwa kuzushiwa tuhuma hizo, Aisha aliyewahi kung'ara katika filamu mbalimbali, alisema hana mpango wa kufanya lolote kwa sababu hataki kugombana na vyombo vya habari, inagwa hakupendezwa na kilichoripotiwa ambacho alidai alikisoma mapema leo.
"Nawapotezea tu sina mda wa kugombana na vyombo vya habari," alisema Aisha Bui, mwanadada aliyewahi kuripotiwa kuolewa na aliyekuwa mfanyabiashara na mdau mkubwa wa muziki nchini, Marehemu Mohammed Mpakanjia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...